Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akizungumza na mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

...............................................................

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Wizara itashughulikia askari wanaochafua Jeshi la Polisi kwa kupitia Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji, ili kurejesha imani ya wananchi kwenye Vyombo vinavyosimamia Ulinzi na Usalama wa mali zao.

Amesema kuwa Tume hiyo ni chombo kinachosimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo hivyo na kwamba Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Makamu wake ni yeye, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hivyo watashugulikia kikamilifu maelekezo aliyoyatoa Rais Samia.

“Kuna maelekezo Mheshimiwa umeyatoa, mimi na Waziri Masauni tutayasimamaia kikamilifu. Ipo Tume ya Utumishi wa Jeshi Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto na Uokoaji, chombo hiki ndio kinasimamia nidhamu za watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.”

Naibu Waziri Sagini amezungumza hayo leo mbele ya mamia ya wananchi wa Mara, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kata ya Kwangwa, Musoma Mjini, Mkoani Mara.

Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka Watanzania kutii sheria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kuwa wateja wa Vyombo vya Dola. Amesema kwamba Vyombo hivyo vinasimamia Sheria na utekelezaji wa Sheria na endapo mwananchi atakiuka sheria za Nchi basi lazima sheria itachukuliwa.

“Niwaombe wananchi hivi ni vyombo vya dola, Sisi tusingependa vyombo hivi vipambane na raia. Usipokuwa, raia atakaye kikuka sheria, raia atakayetenda vitendo vya uahalifu, atakaye mnyima mwenzake amani atakuwa tuu mteja wa Polisi, na baadae Mahakama, mwishowe Magereza”
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: