Mratibu wa Mradi wa Shirika la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF)  Benard Maira, akizungumza na viongozi wa vijiji wilayani Ikungi mkoani Singida wakati wa mdahalo uliohusu haki za binadamu na namna ambavyo matukio ya ukatili wa kijinsia yanavyoshughulikiwa uliofanyika jana.
Mshauri wa Masuala ya Sheria wa shirika hilo na Mratibu Msaidizi wa mradi huo , Paul Kigeja akitoa mada kwenye mdahalo huo.
Afisa Ustawi wa Jamii  Wilaya ya Ikungi, Haroun Yunus Haroun akizungumza kwenye mdahalo huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Siuyu, Rebeca Ngubila akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwakilishi wa Kijiji cha Damankia Andrew Mubila akichangia jambo kwenye mdahalo huo.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mwakilishi wa Kijiji cha Munkinya, Ally Mdimi akizungumza.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Mdahalo ukiendelea.
Taswira ya mdahalo huo.
Majadiliano katika vikundi yakiendelea.
Majadiliano katika vikundi yakiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA  la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) kupitia mradi wa ‘AWARE 2020’ limewakutanisha viongozi wa wilaya na vijiji wilayani Ikungi Mmkoani Singida na kufanya mdahalo uliohusu haki za binadamu na namna ambavyo matukio ya ukatili wa kijinsia yanavyoshughulikiwa.

Malengo makuu ya Taasisi hiyo ni kujenga uwezo wa shirika na wadau katika kupunguza umaskini na kuleta maendeleo, kutoa huduma za afya na kufanya utetezi wa haki kuhusu usawa wa kijinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine athirika.

Akizungumza jana katika mdahalo huo Mratibu wa Mradi wa Shirika hilo Benard Maira alisema kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022 SPRF kwa kushirikiana na Foundation For Civil Society na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanatekeleza Mradi wa " Utetezi wa Haki za Mwanamke na Mtoto wa kike dhidi ya adhari zitokanazo na mila na desturi kandamizi hasa ukeketaji,ndoa na mimba katika umri mdogo kwenye vijiji vinne ambavyo ni Unyankhanya, Siuyu vya Kata ya Siuyu, Munkinya na Damankia vya Kata ya Dung'unyi katika kata hiyo.

Maira aliwataja washiriki wa mdahalo huo kuwa ni Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo, Polisi Dawati la Jinsia, Maafisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Siuyu na Dung'unyi, Watendaji wa Kata ya Siuyu na Dung'unyi, Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji vya Unyakhanya, Siuyu, Munkinya na Damankia na viongozi wa dini kutoka katika vijiji hivyo.

Alitaja washiriki wengine kuwa ni Wazee wa kimila, Ngariba na wawakilishi wa watu wenye ulemavu.

Alisema lengo kuu la mdahalo huo ni kujadiliana kuhusu masuala ya haki za binadamu, ukatili wa kijinsia na namna yanvyoshughulikiwa na kuwa ni mdahalo utao ibua changamoto zilizojitokeza kupitia mradi huo na kuweka mikakati na kutoa mapendekezo na maazimio ya nini kifanyike kukomesha ukatili wa jinsia katika jamii.

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa shirika hilo na Mratibu Msaidizi wa mradi huo , Paul Kigeja akizungumza kwenye mdahalo huo wakati akitoa mada ya Haki za Binadamu alisema ni kutambuliwa na kulindwa na haki za msingi ni kulinda utu na heshima ya mtu na kuwa zikikiukwa zinakuwa zimetweza.

Alitaja sifa kadhaa za haki za binadamu kuwa hazigawanyiki,Zinategemeana,kushirikiana na nyingine ni stahiki ya kupata haki bila kujali jinsia ya mtu, nafasi yake na mambo mengine kama kabila, utaifa, hali ya maisha yake na utu wake.

Mmoja wa washiriki wa mdahalo huo Ally Mdimi kutoka Kijiji cha Munkinya , alisema mafunzo waliyoyapata kutoka katika shirika hilo yamesaidia kuibua matukio ya ukatili wa kijinsia hasa yanayowahusu watoto, wanawake na wanaume na baadhi ya watuhumiwa wakichukuliwa hatua mbalimbali huku wengine wakiwa gerezani wakitumikia vifungo vyao.

Akizungumzia kundi la wanawake amesema wamekuwa wakipigwa na moja ya tukio hilo ni la baba kumpiga binti yake mjamzito ambaye hivi sasa yupo gerezani akitumikia kifungo cha miezi sita.

Alitaja tukio la pili ni la kijana mmoja kumtishia dada kwa silaha ya jadi na sasa yupo gerezani akitumikia kifungo baada ya Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na polisi kushughulia suala hilo.

Alitaja tukio lingine kuwa ni kundi la watoto kuathirika kwa kunyimwa haki ya kusoma kwani alikuwepo baba mmoja ambaye alikuwa hataki watoto wake kuhudhuria shuleni na kuwapangia kazi mbalimbali lakini baada ya kubanwa na kufuatiliwa mara kwa mara na Serikali ya kijiji na timu iliyopata mafunzo kutoka SPRF watoto sasa wanakwenda shuleni kama kawaida.

Alisema sababu kadhaa za kukithiri kwa matukio hayo katika kijiji hicho kuwa ni ni ulevi wa kupindukia,urafi na ukosefu wa elimu na hofu ya Mungu.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: