Na Joel Maduka Geita 


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina amefanya ziara ya siku moja Wilayani Chato yenye lengo la kutoa salamu za pole kwa familia ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli.


Akiwa nyumbani kwa hayati Dkt. John Pombe Magufuli Dkt. Akinwumi Adesina amesema amefika nyumbani kwa hayati Magufuli kutokana na urafiki mkubwa aliokuwa nao yeye na hayati Rais Maguli pamoja na kutambua mchango mkubwa ambao hayati Magufuli aliutoa kwa watanzania na kwa watu wengine.


 “Rais Magufuli alikuwa mfano mzuri kwa viongozi barani Afrika, aliwapenda watanzania na waafrika wote kwa moyo wake wote” alisema Dkt. Adesina.


Rais wa AfDB amesema pamoja na kuodokewa na Rais Magufuli anafarijika kuona Tanzania bado ipo kwenye mikono salama chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anaendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na hayati Magufuli.


Dkt. Akinwumi Adesina amemshukuru Rais Samia kwa ushirikiano na kumruhusu kufika Wilayani Chato kwa ajili ya kutoa salamu za pole.


Dkt. Akinwumi Adesina na ujumbe ulioambatana naye wamerejea jijini Dar es Salaam.

Share To:

Post A Comment: