Julieth Ngarabali.Pwani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Ridhiwan Kikwete amesema Serikali imetoa muda wa siku 60 kuanzia Februari 05 mwaka huu kuhakikisha wale wote waliopimiwa viwanja wanawasilisha maombi ya kumilikishwa.
Amesema kwa wale wananchi wenye milki za ardhi nao pia wanatakiwa wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi ndani ya muda huo uliyotolewa.
"Mmiliki ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa,Serikali itachukua hatua kisheria ikiwemo kufuta umiliki,kupiga mnada na kumilikisha viwanja vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji "amesema Ridhiwan
Ridhiwan ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amebainisha kuwa zoezi la kuchukua sheria dhidi ya wasiolipa kodi litaanza rasmi Aprili 04 (nne) mwaka huu
Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa Wizara yake kwa sasa inakumbusha Umma kwamba ni wajibu wa kisheria kwa wale ambao ardhi zao zimepangwa na kupimwa kuwasilisha maombi ya kumilikisha ardhi kwa Kamishna wa ardhi kwa ajili ya kumilikishwa.
Post A Comment: