Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na wananchi wa Bunda, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo,Viwanja vya Sabasaba Miembeni, Wilaya ya Bunda,Mara.Amewataka kuwa raia wema kwa kuepuka vitendo vya kiuhalifu.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi Mikoani kutumia wataalumu wao hadi wa ngazi ya tarafa kudhibiti matukio ya mauaji yanayotokea nchini.Amesema hayo leo,kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika, Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini akizungumza na wananchi wa jimbo lake la Butiama baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan,Wilaya ya Butiama alipokuwa njiani kuelekea Wilaya ya Bunda,Mkoani Mara leo.

................................................

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kutumia wataalamu wao hadi wa ngazi ya tarafa kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyotokea nchini.

Amesema kwamba haiwezekani Jeshi la Polisi kumwachia Rais Samia kuzungumzia jambo ambalo Makamanda wa Polisi wapo na wanauwezo wa kulisimamia kwenye maeneo yao.

“Niwaombe Makamanda wa Polisi Mikoa yote, tumieni wataalamu mlio nao kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyotokea nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi Hamad Masauni na mimi, haturidhishwi kabisa kumwachia Mhe. Rais kuzungumzia jambo ambalo mpo na mna uwezo wa kulisimamia”

Naibu Waziri Sagini amezungumza hayo leo mbele ya mamia ya wananchi wa Bunda, baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Shule ya Msingi Miembeni, Wilaya ya Bunda Mjini, Mkoani Mara.

Aidha akizungumza na wananchi hao amewataka kuwa raia wema na kuepuka vitendo vya kiuhalifu kwa sababu Jeshi la Polisi halitawafumbia macho wahalifu. Amesema Jeshi hilo linawataalamu wa Upelelezi, wataalamu wa Jinai kwahiyo wahalifu wote watashughulikiwa.

“Mheshimiwa Rais kwa siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya ovyo yanayodhalilisha utu wetu kwa baadhi ya watu kuwaua wenzao. Jambo hili halikubaliki. Ni aibu kuwa na taifa la watu wanachinjana tena wengine ndugu kwa ndugu na wengine wakwe, ni fedheha ambayo haiwezi kuvumilika”

Pia Naibu Waziri Sagini amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu ujenzi wa Ofisi za Makamanda wa Polisi nchini. Amesema ujenzi huo utaimarisha mazingira ya kazi ili wataalamu waweze kufanya kazi zao vizuri.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: