Na Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dr Kundo Andrea ameyataka makampuni ya utoaji huduma za mitandao ya simu ikiwemo kampuni ya Tigo kuhakikisha yanasimama katika nafasi zao ili kuwezesha wananchi kuweza kuondokana na changamoto ya maeneo ambayo mitandao inasuasua.



Mhe. Kundo Naibu Waziri ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea mkoa wa Tabora katika kuhamasisha jamii juu ya matumizi sahihi ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na elimu ya anuani na makazi ambapo amesema, makampuni ya simu ni njia mojawapo na kubwa ya kuwezesha zoezi la serikali kufanikiwa.



Akizungumzia hatua zinazochukuliwa na kampuni ya Tigo kuhakikisha mawasiliano yanaimarika, Meneja wa utoaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi wa kampuni ya Tigo Bw. Lugutu Lugutu amesema, suala la mawasiliano kampuni inaendelea kuliimarisha mkoani Tabora.

Aidha akijibu baadhi ya maswali ya wananchi hususani yaliyoulizwa juu ya vifurushi kuisha kwa haraka, Meneja wa Tigo mkoani Tabora Bw. Lugutu Lugutu, amewataka wananchi kujiunga na vifurushi vya halichachi ili kuepuka muda wao kupotea.




Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa mawasiliano kwa wote, UCSAF, Pro John Nkoma na mtendaji mkuu wa UCSAF, Mhandisi Justina Mashiba wameyapongeza makampuni yanayoendelea kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma sahihi na kwa wakati.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: