MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira akizungumza wakati wa kikao hicho |
Waziri
wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalumu
Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua kikao hicho |
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati wa kikao hicho |
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bata
(NGOs) Neema Lugangira ameshiriki kikao kazi cha Wadau kwa
ajili ya kuweka Mkakati wa kuimarisha Utekelezaji wa Afua za Kutokomeza
Ukatili wa Dhidi ya Wanawake na Watoto - MTAKUWWA
Kikao
hicho ambacho kilifanyika Jijini Dodoma na kilihudhuriwa na wadau
mbalimbali na kufunguliwa na Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalumu Mhe Dkt. Dorothy Gwajima
ambapo Mbunge Lugangira aliziomba Mamlaka husika kuhakikisha Eimu ya
Ukatili wa Kijinsia inafika kwa Jamii nzima.
Ikiwemo
kuangaliwa kwa umakini kuhakikisha Vyumba vya Madawati ya Kijinsia
visiwe ndani ya Jengo la Polisi badala yake kuandaliwe utaratibu mzuri
ambao utakuwa ni rahisi kwa wananchi kuweza kufikia kwenye maeneo hayo
maana hivi sasa ni ngumu sana kwa mtu aliyefanyiwa Ukatili wa Kijinsia
au Mzazi wa Mtoto akiyefanyiwa Vitendo vya Ukatili wa Kijinsi kupokelewa
Polisi na mbele ya kila mtu aeleze shida yake alafu aingie ndani ya
Polisi apelekwe chumba chenye Dawati la Kijinsia, haya sio mazingira
rafiki.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho Mbunge Neema alisema ni muhimu pia MTAKUWWA
itambue kwamba Ukatili wa Kiinsia Mtandaoni unavyopelekea kuwafanya
Vijana wa Kike, Wanawake na hata Viongozi Wanawake wakiwemo Wanasiasa
Wanawake washindwa kutumia Mitandao ya Kijamii ipasavyo kwa kujiepusha
na Ukatili huo.
Alisema
wakati umefika MTAKUWWA itambue pia Masuala ya Afya ya Akili na hilo ni
jambo la kudharura kwa kuzingatia matukio mengi ya ukatili wa Kijinsia
ambayo ni katika ya visababishi ni pamoja na Msongo wa Mawazo .
Awali
akizungumza wakati akitoa hotuba yake Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalumu Mhe Dkt. Dorothy Gwajima
alikubaliana na Ushauri wa Mbunge Lugangira hivyo kuelekeza Wizara na
Wadau washirikiane katika kuimarisha maeneo haya muhimu yaliyoainishwa
na Mhe Neema Lugangira.
Post A Comment: