Raisa Said, Lushoto.


Mkuu wa Wilaya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro ametangaza msako mkali kuwakamata wazazi na walezi wanaoshiriki kuwaaachisha na kuwatorosha watoto wao shule kwaajili ya kwenda kufanya kazi za ndani .

Mkuu huyo wa Wilaya, akieleza kusitikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wazaz kushiriki katika utoroshwaji wa wananfunzi wa kike na huku wakienda wenyewe kutoa taarifa kwenye shuke husika, aliwaagiza waagiza wenye viti na watendaji wa vijiji kufanya msako huo mara moja na kukamata wazazi na walezi hao.

Lazaro alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha wadau wa elimu kata ya Mponde, kilichofanyika Shule ya Sekondari ya Chai..

“Nitakula sahani moja na wazazi wa namna hiyo kwa sababu wanarudisha nyuma maendeleo ya watoto hao na kukatisha ndoto za baadae za watoto wao,” alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alitoa ushuhuda wa tabia hiyo aliposema kuwa kuna mzazi alifika ofisini kwake na kudai kuwa mtoto wake amepotea nay eye aliamua kumuweka ndani. “Cha ajabu ni kuwa baada ya kumlazimisha apigie simu ndugu zake ili mtoto arejeshwe na mtoto alipatikana baada ya muda mfupi,” alisema.

Aliagiza kuwa wazazi au walezi waliowatorosha watoto wao wachukuliwe hatua hkali za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa. Lazsro aliagiza kuwa watakaokaidi wapelekwe ofisi za watendaji kata ili wapelekwe Wilayani kwa hatua zaidi.


Aliafafanua kuwa kuwa faini hizo zitakuwa mapato halali ya kata na Halmashauri.

Lazaro alisema ni aibu kubwa kwa wazazi kuwatorosha watoto shule na kuwapeleka Mombasa na maeneo mengine wakati serikali inatoa elimu bure na huku Rais Samia akiendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya shule zote ikiwemo kujenga madarasa.

Mkuu huyo pia aliagiza wenyeviti hao waitishe mikutano ya serikali za vijiji kwa ajili ya kukubaliana kwa pamoja viwango vya faini zitakazokuwa zinatozwa wazazi ka kosa la utoroshaji.

Alisisitiza kuwa pamoja na faini hizo ni lazima watoto waliotoroshwa watafutwe walipo na kurudishwA kwa ajili ya kuendelea na masomo yao ili watimize ndoto zao.

Mkuu wa Shule ya Msingi Mponde Maimuna Perembo alisema alithibitisha kuwepo kwa utoroshaji na kuwaachisha shule watoto hasa wa kike. Alisema hatankwenye shule shule hiyo tatizo hilo lipo.

“Kuna kipindi nilipokea mzazi ambaye alifika kutoa taarifa juu ya kupotea kwa mtoto wake kumbe baada ya uchunguzi ilionekana mtoto wake amepelekwa Mombasa kufanya kazi za ndani,” slisema.

Alimwomba Mkuu wa Wilaya awasaidiekukomesha ttizo hilo kwa sababu wazazi wengi wanasingizia watoto wao wamepotea kumbe wanatumia mbinu hiyo kujihami wasichukuliwe hatua za kisheria.

Nae Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Kwemhafa , Alex Mponda alieleza kwamba kitongoji chake kinaongoza kwa Wazazi kuwatorosha watoto hivyo akaomba kikao hicho kitoe maazimio ya kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani wazazi hao ili kukomesha jambo hilo la utoro katika maeneo yao.

Awali akisoma taarifa ya hali ya elimu katika kata hiyo, Mratibu wa Elimu Kata ya Mponde, Grace Sowa alisema kata hiyo ina jumla ya wanafunzi 2,462 wa shule za msingi huku sekondari ikiwa na jumla ya wanafunzi 519. Alisema idadi ya walimu wa sekondari ni 25 na msingi ni 37.

Akizungumzia kuhusu ufaulu alisema kuwa kwa miaka mitatu hali ya taaluma ilikuwa wastani lakini kwa miaka hii miwili iliyopita (2020 na 2021), hali ya ufaulu imeshuka kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo utoro wa wanafunzi,ukosefu wa chakula cha mchana na mwitikio mdogo wa wazazi katika kufuatilia maendeleo ya kitaaluma ya watoto wao.

Hata hivyo Diwani wa kata hiyo ya Mponde, Richard Mbughuni alisema atahakikisha maazimio yaliyotolewa katika kikao hicho cha wadau yanazingatiwa kwa lengo la kukomesha tabia hiyo pamoja na kuongeza ufaulu katika kata hiyo.


Share To:

Post A Comment: