MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akizungumza  Bungeni Jijini Dodoma leo February  11,2022
MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akisisitiza jambo  Bungeni Jijini Dodoma leo February  11,2022


NA MWANDISHI WETU, DODOMA.

MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira ameiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake wa kuondoa masuala ya usalama wa chakula kutoka Wizara ya Afya na kuipelekea kwenye  eneo la mambo ya viwanda na biashara warudi kwenye best practice.

Aliyasema hayo Bungeni leo Ijumaa tarehe 11 Februari 2022 Jijini Dodoma ambapo alisema kwa sababu duniani kote masuala ya usalama wa chakula yanaratibiwa na chini ya wizara ya afya kwa maana chini ya mamlaka ya kudhibiti ubora wa chakula na dawa na hata kwa Tanzania miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya hivyo chini ya TFDA.

Mbunge Neema alisema hata nchi za Afrika Mashariki zilikuja nchini kuja kujifunza lakini miaka ya karibuni serikali ilivunja mamlaka hiyo na badala yake kuunda TMDA na jukumu la usalama wa chakula wakaliweka chini ya Shirika la viwango (TBS) sasa jambo hilo limeweka maisha na afya za watanzania herani.

Alisema anasema hivyo kwa sababu TBS ina jukumu la kuangalia ubora wa matairi,misumari,mabati na nk na hapo hapo  ipewe jukumu la kuratibu na kudhibiti ubora na usalama wa chakula na hao hao ndio wanatoa kibali kwa wazalishaji wa chakula .

“Na hao hao waende kuangalia kile kibali kimekidhi kutakuwa na mgongano wa maslahi, Mh Naibu Spika kuna jambo mahususi lilijitokeza ambalo ni dhihiri kwamba TBS haiwezi kuendelea kubeba jukumu la usalama wa chakula “Alisema

“Kwa mfano mwaka jana Octoba 2021 Shirika la chakula na madawa la Kenya lilitangaza kwamba linarudisha juice aina ya Seresi za Apple ambazo zilikuwa na aina moja ya sumu kuvu ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu mpaka siku hiyo kwa Tanzania TBS bado ilikuwa haijasema chochote”Alisema

Mbunge huyo alisema na gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na anakumbuka  alisema mpaka muda wa Octoba 14 mwaka 2021wamejiridhisha  juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na wanaendelea kufuatilia na wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa .

Alisema hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa TBS waliwadanganya watanzania  kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski kimoja Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye Barcode zile zile zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na kumtumia waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji.

Aliongeza kwamba baada ya Waziri huyo kupokea alisema ataifanyia kazi  hilo linaonyesha TBS hawakuchukulia kwa umakini jambo la usalama wa chakula na hawana muda wa kuangalia usalama wa chakula na wanahatarisha maisha ya watanzania kwa kuendela kulimbikiza mambo mengi ambayo mengine hayaendani na usalama wa chakula

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: