Na. Asila Twaha, TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt. Grace Magembe amewataka  Maafisa Wasimamizi wa fedha  katika  Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa kuwa na malengo yanayoendana na Serikali kwa kutumia mashine za kieletroniki  katika ukusanyaji wa mapato. 


Dkt.Grace  ametoa wito huo  leo Jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Mradi wa Fedha za Umma “Public Finance Management Reform Program Implementation Committee” (PIC) kilichowakutanisha watalaam wa masuala ya fedha katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Mamlaka za Serikali za Mitaa  na Wadau wa Maendeleao.  


Amesema, ili Halmashauri ziweze  kusimama na kujitegemea   lazima watalaam  hao  wasimamie  ukusanyaji wa mapato  ya Halmshauri kwa kutumia  mashine za kieletroniki,  amesema usimamizi wa fedha za Umma unaendana na uwepo wa maendeleo katika eneo husika hivyo  ni lazima kuzingatia  sheria katika ukusanyaji ili wananchi wawe ni wanufaika wa maendeleo.


Akielezea mradi wa PIC ulivyosaidia kusimamia fedha za Umma katika ukusanyaji wa mapato ya Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema, zipo Halmashauri ambazo vyanzo vya mapato vimeongezeka sababu ya  kutumia teknolojia za kisasa  ikiwemo  mifumo iliyowekwa katika ukusanyaji wa mapato katika kutumia mashine za kieletroniki.


Ametoa rai kwa wataalam wa fedha katika Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa katika ukusanyaji wa mapato kuepuka kutokutumia mashine kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato sababu kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria lakini pia kuenda kinyume na malengo ya  Serikali katika kuwaletea maendeleo ya wananchi.

Share To:

Post A Comment: