Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida Innocent Msengi, akizungumza leo kwenye baraza la madiwani ambalo limepitisha rasimu ya bajeti ya zaidi ya Sh.41.1 Bilioni. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Michael Matomora na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Monica Samwel.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Michael Matomra akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Sango Songoma akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Madiwani wakiwa kwenyekikao hicho.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Henry Makwasa, akijitambulisha kwenye kikao hicho baada kuhamia wilayani humo hivi karibuni.
Kikao kukiendelea.
Madiwani wakipitia makabrasha kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya hiyo Asia Matitu akijitambulisha kwenye kikao hicho baada ya kuhamia wilayani humo hivi karibuni akitokea mkoani Kigoma.
Taswira ya kikao hicho.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Daudi Madelu akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Samuel Ashery akizungumza kwenye kikao hicho.
Wataalamu na wakuu wa  idara mbalimbali wa halmshauri hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.
kikao kikiendelea


Na Dotto Mwaibale, Iramba


BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limepitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.

Mpango huo umepitishwa katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika jana  katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo ambapo limepitisha Rasimu ya Bajeti yenye makisio yenye thamani ya Sh.41,163,999,997.24 Bilioni katika bajeti hiyo kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

 Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael Matomora alisema katika rasimu fedha kutoka mapato ya ndani Sh.5,384,746,533.24, ruzuku ya Serikali ni 25,407,823,634.10 huku wahisani ikiwa ni Sh10,371,426,830.

Alisema mwaka ujao wa fedha wa 2022/ 2023 halmashauri hiyo imekisia kutumia jumla ya 41,,163,996,997.24 kutokana na vyanzombalimbali.

Alisema kutoka mapato ya ndani wametenga Sh. 23,,526,000, matumizi ya kawaida Sh.2,143,494,086.24, miradi ya maendeleo,3,217,726,444 jumla ya mapato ya ndani ikiwa ni Sh.5,384,745,533.24.

Akielezea ruzuku ya Serikali alisema mishahara ni Sh.20,418,014,391, matumizi ya kawaida Sh. 1,000,776,000,miradi ya maendeleo Sh.3,989,033,243 jumla ikiwa ni Sh. 25,407,823,634.

Alitaja fedha kutoka kwa wahisani ni Sh.10,371,426,830 huku jumla yake ikiwa ni Sh. 41,163,996,997.24.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba Innocent Msengi aliwapongeza madiwani kwa kupitisha rasimu hiyo ambayo ameitaja kuwa ni ya kipekee na ya mfano.

"Nitumie nafasi hii kuwapongeza madiwani kwa kuandaa rasimu hii nzuri na ya kipekee hivyo nawaombeni mkaitekeleze katika kukusanya mapato ili tuwenze kusonga mbele" alisema Msengi.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda alishukuru madiwani hao kwa kupitisha rasimu hiyo na akatumie nafasi hiyo kuwaomba madiwani hao kwenda kuhimiza wananchi wao kujitokeza kwa wingi wakati wa zoenzi ya sensa ya watu na makazi na anuani za makazi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba aliwaomba madiwani hao kwenda kuzisimamia vizuri fedha hizo na akataka kuwepo na mashindano ya kuwashindanisha kwa utendaji kazi wao na washindi wapatiwe zaidi pamoja na wananchi wao waliofanya kazi husika.

 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: