Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Miburani wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, Amiri Matimbwa amewataka viongozi wa matawi na mashina katika Kata hiyo kuhakikisha wanahamasisha kikamilifu Wanachama kujiandikisha katika mfumo wa kadi za kieletroniki.


Matimbwa ametoa malekezo hayo leo February 26, 2022 alipokuwa anazungumza kwenye Mkutanao Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Miburani uliofanyika kwenye ukumbi wa Idd Nyundo, Temeke.


"Malengo na mikakati yetu kipindi hiki ni kuhamasisha Wanachama wetu kujisajili katika mfumo wa kadi za kieletroniki na kusajili Wanachama wapya. 


"Hivyo niwaombe sana viongozi wa matawi na mashina kuhakikisha mnajitoa kuhamasisha Wanachama kujiandikisha katika mfumo huu wa kieletroniki ikiwa ni kurahisisha kuwahudumia na kuwatambua wanachama wa CCM kwa urahisi.” alisema Matimbwa


Kadi hizo zilizinduliwa rasmi Februari 5, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan.


Mchakato wa kadi hizo za kieletroniki ulianza Disemba 2018 ambapo mpaka sasa zaidi ya  wanachama milioni 2,077,182 wamejiandikisha.

Share To:

Post A Comment: