Ni matumaini yangu unazidi kuelimika kwa namna moja ama nyingine. Katika makala yetu ya leo nitakwenda kueleza kuhusu siri za mafanikio zilizojificha ambazo wengi wetu huenda tukawa tunazijua au tukawa hautuzifahamu pia.

Kimisingi siri hizi ndizo zitakazokufanaya wewe uweze kutoka hapo  ulipo na kuzidi kusonga mbele kwa maana ya kuwa na mafanikio zaidi. Mafanikio ninayaongelea hapa ni yale ya kila sekta aifanyayo mwanadamu.

Mafanikio ndio msingi mkubwa kwa kila mwanadamu.  Watu wengi huwa tunapata nafasi mbalimbali za kufanya kazi lakini wengi wetu tunashindwa kuzitumia nafasi hizo.  Mfano leo hii umepata ajira mahali Fulani wengi wetu hufanya kazi ilimradi tu badala ya kuonyesha uzoefu  na ubunifu zaidi ulionao.

Ngoja nikusimulie kisa kimoja ili utambue siri hizo zilizojificha za kimafanikio;  Kuna mwindaji mmoja katika kijiji Fulani alikwenda kuwinda wanyama katika msitu ambao upo mbali na makazi yake. Baada ya kuwinda kwa muda mrefu  alizunguka sana huku na huko lakini hakupa kitoweo kwa siku ile.

Siku iliyofuata hukukataa tamaaa alikwenda tena msituni kwa ajili ya zoezi la uwindiji. Alizunguka sana siku hiyo lakini hakupata chochote , ilipofika majira ya saa nane mchana mwindaji Yule kwa kuwa alikuwa amechoka sana alimpasa apumzike katika msitu uleule ili akusanye nguvu za kuendelea kuwinda.

Baada ya muda mchache aliendelea tena  na zoezi kuwinda bila kukata tamaa lakini hukupata chochote. Aliendelea tu kuwinda na kujisemea ndani ya moyo wake kwamba ‘naendelea kuwinda sikati tamaa kama ilivyotekea  jana.

Ghafla wakati akiendelea  kuwaza hayo katika akila yake  alitazama chini na kuona mayai mawili ya ndege aina kanga. Mwindaji Yule  Alifurahi sana  kwa kuwa alikuwa amezunguka sana , aliamua kuchukua mayai yale mawili.  Yai moja akalishika upande wa mkono kulia na yai jingine akalishika upande wa mkono kushoto.

Badaa ya muda mfupi alianza kupanga mipango juu ya mayai yale.  Alianza kwa kusema maneno haya mayai haya nitakwenda kuchanganya na mayai kuku wangu, mwisho wa siku watazaliwa kanga wawili, kanga hao nao watazalina watakuwa wengi zaidi, kwa baada ya miaka kama 20 nitakuwa mzalishaji mkubwa wa kanga katika kijiji hichi na mkoa kwa ujumla, hivyo nitakuwa na wateja wengi sana, nitapata hela nyingi sana, niatajenga nyumba nzuri na yenye kila kitu cha kisasa, nitanua magari mengi kwa ajili kutembelea , nitanunua mifugo mingi kwa ajili ya kufuga na kupanga mambo mengine mengi.

Kumbuka ya kuwa wakati anapanga hayo mayai yalikuwa bado mikonono mwake. Baada ya muda mchache baada ya kupanga mipango yake juu mayai,  alijiona jinsi atakavyokuwa tajiri na atakavyokuwa tofauti na wanakijiji wengine, furaha ilimizidi na kusahau kuwa ameshika mayai mikononi mwake alipiga makofi na kusema Mwenyezi mungu nisaidie baada ya kupiga makofi mayai yale mawili yalivunjiaka na ndoto zake zote zikawa zimeishia pale. Furaha yake juu ya mipango  ya maisha ikamfanya ndoto zake ziishie pale.

Kisa hiki kinatufundisha baadhi ya mambo yafutayo;
Kuna uwezekano mkubwa sana Furaha ikizidi sana inakufanya ushindwe kutimiza malengo na ndoto ulizokuwanazo. Unaweza ukasema afisa muongo ila huo ndo ukweli. Ni watu wangapi leo hii walikuwa na fulaha sana siku ya sherehe mbalimbali na leo hii ni vilema?  ikifuatilia juu ya hilo utakuta ni wengi mno na wengi ndoto zao zimeishia hapo. Mtu anakuwa na furaha iliyozidi mwisho wa siku anajipongeza kwa kunywa pombe matokeo yake furaha inageuka  na kuwa majuto.  Ukiona  ya kuwa una furaha fanya kitu cha maendeleo kuliko kufanya mambo ambayo yatakughalimu maisha yako yote.

Kisa hiki pia kinafundisha kutokukata tamaa kwenye mambo mbalimbali.  Siku sote zipo changamoto ambazo huwa zinaingilia mambo yetu ya kimafaniko. Kama tulivoona katika kisa hicho naamini ya kuwa mwindaji ana nafasi nyingine ya kutazama ni vipi malengo yake yanaweza kutimia kwa kuangalia fursa zingine zilizopo?

Daima tukumbuke ya kuwa kwa kawaida binadamu wote tuna malengo na ndoto  kubwa za kimanikio ila tatizo ndoto hizo huja kwa kualibiwa na kitu kimoja tu. Hivyo ni vyema kuepuka na kitu hicho ambacho kitakufanya usiweze kutimiza malengo yako. Kila siku tukumbuke ya kuwa sio kila furaha ikizidi sana itakufanya ushindwe kusonga mbele.
Share To:

Post A Comment: