Mwamvua Mwinyi, Pwani


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa,Daniel Chongolo ametoa wito kwa wananchi wa Kibaha ,Pwani kutumia fursa ya miundombinu rafiki kuelekea Chuo cha Uongozi Cha Mwalimu Nyerere kujikomboa kiuchumi ili kujiletea maendeleo.


Aidha amekemea uharibifu wa miundombinu ya barabara na kuelekeza barabara ya Ukombozi kuelekea chuoni hapo, ilindwe na kuwekewa mazingira mazuri ya kudumu kwa maslahi ya vizazi vijavyo.


Akizindua barabara ya Ukombozi kuelekea Chuo cha uongozi kikubwa Afrika, Kibaha yenye takriban kilometa 1.8 , Chongolo alisema ,ni wakati wa kutengeneza program ya kutumia chuo hicho kwa kuzalisha kisasa kwa lengo la kufungua milango ya kimaendeleo.“Leo tmekuja kwa kazi moja kazi ni kesho,sisi tumekuja kufungua njia, kesho ni uzinduzi wa Chuo”


“Ukombozi tulishakamilisha sasa tuna historia , tunahitaji ukombozi unaoenda pamoja na uchumi katika mataifa yetu” Kwahiyo wito wangu kwa wana kibaha tumeleta chuo,ni lazima mtengeneze programu kwenye maeneo yenu kujikwamua kupitia chuo hiki katika maeneo mahususi.”


“Hatutogemei kuona uvuvi wa kienyeji,kulima kienyeji kusubiri nazi ianguke kujitengenezea mapato,leo tumezindua barabara mwanzo ilikuwa shida kupitika kirahisi ,natoa rai itunzwe barabara kwa manufaa ya vizazi vijavyo”


Chongolo alitaka miundombinu itunzwe watu waache kumwaga taka ovyo,malori yaachwe kumwaga mchanga ili fedha ya marekebisho iweze kuelekezwa katika matumizi mengine ya kimaendeleo.
 

Chongolo alisema kuwa barabara hiyo ya lami itafungua njia za uchumi kwa wananchi wa eneo hilo .


“Mnapaswa kuitunza barabara hii ili iweze kuwaletea manufaa kiuchumi kwani inarahisisha ufikaji wa maeneo mbalimbali ambapo zamani hakukuwa na lami ambayo imekuwa mkombozi alisema Chongolo.


Chongolo alibainisha, barabara hiyo ni muhimu ambapo inasikitisha kuona baadhi watu wanaweka takataka hali ambayo haionyeshi kujenga mazingira mazuri kwa barabara hiyo ambayo inaelekea kwenye chuo hicho kilichojengwa kwa pamoja na vyama vya CCM Tanzania , ZANU PF Zimbabwe, FRELIMO Msumbiji, ANC Afrika Kusini, MPLA Angola na SWAPO Namibia.


Wakishuhudia uzinduzi huo,makatibu wakuu wa vyama rafiki washirika ikiwemo ZANU PF cha Zimbabwe, MPLA cha Angola, SWAPO Namibia FRELIMO Msumbiji na ANC Afrika Kusini, Katibu wa Chama Cha SWAPO ,Sophia Shinengwa yeye alipongeza njia iliyoachwa na Magufuli, na kuimarisha mahusiano yaliyopo katika vyama sita washirika wa Ukombozi.


Sophia alifafanua, Jina la Mwalimu Julius Nyerere limetumika katika Chuo hicho ambapo zile fikra zake za kulikomboa Bara la Afrika zitatekelezwa kwa vitendo kwa sababu watapatikana viongozi ambao watakuwa na uzalendo wa hali ya juu kwa kuwa mafunzo yatayoakisi Itikadi na falsafa za Mwalimu Nyerere.
Mwakilishi kutoka ANC Sibongile Desani ANC alisema Tanzania ni nchi ya kuigwa ,na uzinduzi wa barabara hiyo unaunganisha uhusiano wa kihistoria.


Alieleza ,Afrika ya Kusini kwa miaka 810 bado inaendelea kuchota hekima katika Taifa hilo huku ikiendelea kupambana na harakati za ukombozi.
Kwa upande wake katibu wa Chama Cha ZANU PF cha Zimbabwe Dk Obeid Mpofu wanapongeza vyama hivyo rafiki vya Kusini mwa Afrika kujenga chuo hicho kuenzi harakati za waasisi wa mataifa yao na kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Mpofu alisema kuwa Tanzania ilikuwa ni muhimili wa Mapinduzi kwa nchi za Kusini mwa Afrika na kuenzi mawazo yake.

Mwakilishi wa chama cha MPLA Manuel Agusto Alieleza, ushirikiano wa vyama hivi unaimarisha mataifa yao kwa kuenzi yale mazuri yaliyoachwa na waasisi.
Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa , Mkoani Pwani (MNEC) ,Hajji Jumaa alishukuru vyama vya Ukombozi kwa kushirikiana kuwezesha ujenzi wa chuo hicho na kuwaomba kuja kuwezesha na sekta nyingine.


Alisema Raslimali za nchi hii zitumike kwa faida na maslahi ya wote .
Uzinduzi wa barabara hiyo,ni muelekeo wa uzinduzi wa Chuo cha Uongozi Kwamfipa February 23 mwaka huu,ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi , katika uzinduzi wa Chuo hicho Cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere Cha Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: