Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi. Janeth Mayanja ametoa saa 24 pekee kwa Wakulima Wavamizi wa Bwawa la Gawlolo lililopo Kijiji cha Gawlolo Kata ya Dirma Wilayani Hanang Mkoani Manyara, waliovamia na kuligeuza Bwawa hilo kuwa eneo la Mashamba jambo ambalo ni kinyume cha sheria na matumizi ya Bwawa hilo linalotakiwa kutumika kwa matumizi ya malisho na upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani.


DC @mayanjajaneth ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya ghafla na kukuta uharibifu huo unaotajwa kuhusisha Watu 31 kutoka kijijini hapo na kuwataka kuchukua hatua mara moja ya kuliacha Bwawa katika matumizi yake ya @mayanjajaneth na endapo watakiuka agizo hilo Jeshi la Polishi kuchukua nafasi yake.


Pia DC @mayanjajaneth ameiagiza halmashauri ya Kijiji  ndani ya siku saba wawe wameunda kamati ya uhifadhi katika eneo hilo kwa usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang ili kulinda na kuhifadhi bwawa hilo kwa masilahi ya Wananchi wa kijiji hicho na vijiji jirani wanaotumia bwana hilo.


Bwawa la Gawlolo lina ukubwa wa Hekari 2000 ambalo hutumika kunywesha  na mifugo  katika vijiji vinne katika kata hiyo ambavyo ni Dumbeta, Mureru, Dirma na Gawlolo. 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: