NA JOEL MADUKA .GEITA 


Wafanyabiashara na Wajasiliamali  wa Soko la Kila siku lililopo katika Kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu Halmashauri ya  Msalala  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamemuomba  Mbunge wa jimbo hilo kuingilia Kati na kutatua changamoto iliyopo kwa sasa ya ubovu wa  miundo mbinu ya soko hali inayopeleka  kuhataharisha maisha yao   kipindi hiki cha msimu wa mvua.Wafanyabiashara wameyasema hayo wakati walipotembelewa na mbunge wa jimbo Hilo ikiwa Ni muendelezo wa kusikiliza kero na changamoto za wananchi wa Jimbo lake.


"Mbunge tunakuomba tusaidie kutatua tatizo hili la ubovu wa soko muda sasa soko letu limekuwa na changamoto ya miundombinu yake kuwa mibovu" Mussa Gadi Mwananchi Kakola.Aidha kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo , Charles Fusi amewatoa ofu  wafanyabiashara wa Soko hilo na kwamba  Halmashauri ipo kwenye mpango wa kujenga Soko Kubwa la kisasa na mpaka Sasa wako kwenye mchakato wa kuanzisha ujenzi wa Soko Hilo la kisasa. Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim Idd amewataka wafanyabiashara hao kuwa  watulivu kwani tayari mchakato umeanza wa  ujenzi wa soko la Kisasa.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: