Kwaniaba ya UVCCM Mkoa wa Mbeya tunaungana na Watanzania wote kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kazi kubwa ya kutuletea maendeleo kwa kipindi kifupi ndani ya miezi 9 ya uongozi wake.


Mama Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Mama Samia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.


Sisi kama Vijana hatuwezi kumuacha peke yake Rais wa Nchi akatishwe tamaa na mtu au kikundi cha watu wachache kwa maslahi yao kisiasa.


Tunampongeza kwa serikali anayoiongoza kukopa fedha toka IMF Trioni 1.3 kwa ajili ya miradi ya ujenzi katika sekta ya elimu, Afya na Maji.

Na maendeleo yanaonekana ikiwa katika hatua ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari na shikizi.


Na serikali ya awamu ya 6 sio ya kwanza kukopa, hivyo tunashangaa kiongozi ambaye anaongoza Muhimili wa Bunge ambalo lina dhamana ya kutunga sheria za Nchi na kupitisha Bajeti Kuu ya Nchi anajitokeza hadharani na kumkosea adabu Mheshimiwa Rais kwa maneno ya dharau na kujimwambafai kuwa anasubiri 2025.


Mheshimiwa Spika Job Ndugai amekosa uhalali wa kuongoza Muhimili wa Bunge hivyo anapaswa kujiuzulu na abaki na uwakilishi wa wananchi wa Kongwa.


Hata huko Kongwa nao wananchi wanapaswa kujiuliza je mwakilishi wao anatosha kwa namna alivyo na tamaa na kauli za kudharau viongozi wenzake, kuidharau Nchi na kudharau maendeleo ambayo yanaletwa na serikali ya awamu ya 6 katika Jimbo na Wilaya ya Kongwa.


Tunamsihi na kwa uharaka Mheshimiwa Spika Ndugai kwa maslahi mapana ya Nchi yetu na Chama chetu ajiuzulu.


Alipo Mama, Vijana tupo.

Tutamlinda kwa maslahi ya umma.


KAULI YETU: KULINDA NA KUJENGA UJAMAA WETU.

Share To:

Post A Comment: