Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu amefanya mazungumzo binafsi na wajumbe wa baraza la vijana la wilaya ya Iringa Mjini chini ya Mwenyekiti wake Ndg Salvatory Ngerera

Katika mazungumzo hayo, Mbunge alijielekeza kuwaasa wajumbe wa baraza hilo kuchukua hatua za kuunda vikundi vya kiuchumi ili wawe sehemu ya kunufaika na fedha zinazotolewa na serikali ya chama chao.


 Mheshimiwa mbunge amechukua hatua hiyo baada ya kuona muitikio wa vijana katika kuunda vikundi hivyo ni mdogo sana, ili hali vikundi hivyo vinathibitika kuwa msaada wa kweli kwa vijana kujikwamua na kujiendeleza kiuchumi.


Mheshimiwa mbunge ametoa rai  kwa vijana hao kuwa ifakapo mwezi wa tano, atakapokuwa na ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo, moja ya mambo ya msingi atakayoyafanya ni kivifuatilia vikundi hivyo vitakavyokuwa vimeundwa na atachukua hatua za kuvisaidia na kuviendeleza kwa jitihada zake binafsi.


Pamoja na mambo mengine, mheshimiwa mbunge pia alizungumzia shughuli zote za maendeleo zinazoendelea katika jimbo la Iringa Mjini na kuwataka wajumbe wa baraza hilo kuwa mabalozi wa mambo mazuri yanayofanywa nae pamoja na madiwani wote kwa kushirikiana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Samia Suluhu HassanShare To:

Post A Comment: