Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoni Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani kwa kosa la kupokea rushwa kwenye mabasi maeneo ya Ipogolo manispaa ya Iringa tarehe 18/01/ 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa kamanda Takukuru Mkoa wa Iringa,Domina Mukama alisema kuwa walimukamata Copro Steven Mchomvu akipokea rushwa kwenye mabasi ambayo yanapita katika barabara ya ipogolo.

Alisema kuwa picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zilipigwa na maafisa wa TAKUKURU mkoa wa Iringa mara baada ya kumkamata askari huyo wa usalama barabarani akipokea rushwa kutoka kwenye basi.

Mukama alisema kuwa polisi huyo bado anashikiriwa na Jeshi la polisi mkoa wa Iringa na taratibu zote zikikamilika atapelekwa ndio watatoa taarifa nini kitafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kuwa walimkuta na kiasi cha shilingi laki moja na nusu pesa tathilimu ambazo alikuwa nazo mfukoni ambazo alikuwa akipokea rushwa kwa magari mbalimbali

Alitoa onyo kwa watumishi wote wa serikali waache mara moja tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa ni kinyume cha sheria za utumishi wa UMMA kama ambavyo walikula kiapo wanapoanza kazi.

Mukama alisema kuwa mara baada ya kumkamata askali wa usalama barabarani copro Steven Mchomvu alimshirikisha OCD wa Iringa kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa pamoja.

Aidha kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Iringa alisema kuwa wamefanikiwa kukagua jumla ya miradi kumi na mbili (12) yenye thamani ya shilingi bilioni saba milioni mia moja themanini na tano elimu mia tano sabini na tisa na kumi na tano (7,135,579,015).

Alisema kuwa miradi hiyo ni ya sekta ya elimu,ujenzi (barabara) na afya ambayo miradi hiyo ilikaguliwa kwa lengo la kujua thamani halisi ya pesa iliyotumika na na ubora wa miradi husika kama inaendana na miradi yote ilikaguliwa na kukuta inaendelea vizuri na kwa ubora unaotakiwa.

Mukama alisema kwa kipindi cha oktoba na disemba mwaka 2021 walipokea jumla ya malalamiko 48 yanayohusiana na rushwa lakini baada ya uchunguzi waligundua kuwa taarifa za rushwa zilikuwa 26 na 22 hazihusiani na rushwa.

 

 

 

 

Share To:

Post A Comment: