Na : Teddy Kilanga,Arusha

Waziri wa nchi,Ofisi ya waziri mkuu,kazi vijana,ajira na watu wenye ulemavu Prof.Joyce Ndalichako amesema serikali imetenga kiasi cha sh.bilioni 5.4 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 50 ya watu wenye ulemavu pamoja na ununuzi wa vifaa visaidizi katika vyuo vikuu na sekondari.



Akizungumza katika hafla iliyoratibiwa na ofisi ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini ya kukabidhi viti mwendo na kadi za bima ya afya kwa watu wenye ulemavu wa wilaya ya Arusha ,Prof.Ndalichako alisema fedha hizo ni za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi uviko 19.



Aidha Prof.Ndalichako alisema serikali imeweza kupunguza adha wa kutembea umbali mrefu kwa jamii  pamoja na watu wenye ulemavu kwa kupata huduma zilizo bora kutokana na ujenzi wa zaidi ya vituo vya afya 200 nchini.



"Pia serikali imeanzisha huduma za afya tembezi lengo ni kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma kama chanjo lakini pia ramani za shule pamoja na majengo yake yamejengwa kwa kuzingatia mazingira ya watu wenye ulemavu,"alisema Prof.Ndalichako.



Alisema vilevile serikali imeridhia na inaendelea kutekeleza mikataba mbalimbali ya kitaifa,kimataifa pamoja na kuandaa sera kanuni na miongozo katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao.



Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Mrisho Gambo alisema  jiji la Arusha linajumla ya watu wenye ulemavu wapatao 1009 kati ya hao wanawake 440 na wakiume 560 ambao wanaulemavu wa aina mbalimbali.



Gambo alisema kupitia ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  waliona wayatambue makundi hayo ya watu  ulemavu pamoja na kutambua changamoto zao na kuweza kuzitatua ikiwa utaratibu huo waliuanza mwaka jana.



"Baada ya kugundua kuna watu wenye ulemavu ambao wanachangamoto za matibabu ikiwa kw mwaka jana walitoa kadi za bima 100 sambamba na viti mwendo hivyo kutokana na changamoto za uhitaji zaidi ikabidi waendelee kuwapa bima watoto wote waliochini ya umri wa miaka 18 muda wa ndani ya miaka mitano,"alisema Mbunge huyo.



Mbunge huyo alisema kwa watu wenye ulemavu wanaohitaji miguu ya bandia wapatao 117 ambao walishapimwa hivyo taratibu zinaendelea za kuikamilisha na ikikamilika watapatiwa.



"Mheshimiwa waziri tulikuwa tunaomba kuna baadhi ya majengo hayana miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwani kuna baadhi ya maeneo wakifika watu hawa hufikia nje na kushindwa kupata huduma kama watu wengine,"alisema Gambo.



Aidha alisema kupitia ofisi ya mbunge kwa kusbirikiana na madau kutoka granmelia hoteli wataonyesha mafano wa ujenzi wa choo cha kisasa cha watu wenye ulemavu katika shule ya msingi kaloleni.



Mratibu wa huduma  za viti mwendo kutoka CCBRT wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro,Neophita Lukilingi alisema vifaa tiba hivyo ni vya gharama ambapo watu wenye ulemavu pekee hawawezi kumudu hivyo wanaomba wadau mbalimbali kujitokeza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu.



"Vile vile tunaiomba serikali itusaidie kuongeza vifaa tiba kwa watu wenye ulemavu ili waweze kuwa na maisha bora kama watu wengine,"alisema Mratibu huyo.



Mkurugenzi mtendaji wa Asasi kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture (TAHA),Jackline Mkindi  alisema hafla hiyo imelenga kugusa wati wenye mahitaji maalumu kwani mara nyingi wamekuwa wakisahau katika jamii kwa kuleta maendeleo shirikishi kwa Taifa wapo watu muhimu.



"Napenda kutoa rai kwetu sisi wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na ofisi ya mbunge wetu juu ya mambo mazuri anayoyafanya mbunge Gambo katika kuyaunga mkono kwa lengo hasa kuleta maendeleo,"alisema Mkindi.



Nao baadhi ya wanufaika wa  vifaa hivyo wameshukuru ofisi ya mbunge kwa upendo na uzalendo aliowaonyesha watu wenye ulemavu wa wilaya hiyo kwani sio kitu rahisi.

Share To:

Post A Comment: