Mwandishi Wetu.

Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na wiki kadhaa tangu kuzinduliwa kwa Promosheni  ya WAJIFTISHE GIFTI JUU YA GIFTI inayoendeshwa  na Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania, Aisha Bakari Hill ameibuka mshindi wa pikipiki aina ya Boxer kupitia KAMPENI YA TIGO "WAGIFTISHE  GIFT JUU YA GIFT" akiwa ni mshindi wa wiki ya saba.

Akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa pikipiki mshindi huyo ameishukuru Tigo kwa kuwajali wateja wake na kuamua kurudisha kwa wateja kupitia zawadi.

"Nilinunua  simu ya Shilingi elfu 89 katika duka la Tigo  na  hatimae baada ya muda Nilipigiwa simu na Tigo kuwa nimeshinda pikipiki nawashukuru Tigo mmesongesha maisha yangu pikipiki hii itaniongezea kipato kwa sababu ntampa mtu afanye kazi ya kusafirisha abiria (bodaboda)". Alisema  Bi. Aisha Mshindi wa Pikipiki.

Meneja Mauzo Ubungo Bwn. Sekirito Karia akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa Wiki ya Saba Bi. Aisha Bakari Hill  Promosheni ya Wajiftishe Gift Juu ya Gift

Akimpongeza mshindi wa pikipiki hiyo pamoja na washindi waliojishindia simu janja Meneja wa Mauzo  Tigo Ubungo, Bwana Sekirito Karia  amesema katika mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali nchini, kampuni ya Tigo imewahakikishia wateja wake kuwa kila mtu anapata nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu zaidi kwa kila ununuzi wa simu za kisasa za ITEL T20 kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote, hivyo akawaomba wateja waendelee kununua simu za ITEL T20 na simu nyingine kutoka maduka ya Tigo nchini kote ili kuingia kwenye droo ya kupata nafasi ya kujishindia moja ya pikipiki  zikiwemo simu janja zinawaniwa katika promosheni hiyo.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: