Mke wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Jesca Thomas (28) ameieleza Mahakama namna walivyokamatwa na mume wake na askari waliokuwa na silaha jijini Dar es Salaam.

Jesca ambaye ni shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita ameieleza Mahakama kuwa alikamatwa na mume wake Mei 27 mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Leo Januari 17, 2022 akiongozwa na Wakili Mosses Mahuna anayemtetea Sabaya, Jesca alijitambulisha mahakamani hapo kuwa ni mke wa mshitakiwa huyo na walifunga ndoa mwaka 2018.

Shahidi huyo amedai mahakamani hapo kuwa walikamatwa wao wawili na baadaye walisafirishwa kupelekwa Arusha.

Baada ya kumaliza kutoa ushahidi alianza kuhojiwa na mawakili wa Serikali.

Hata hivyo mawakili wa Serikali hawakumaliza kumhoji ambapo wataendelea kesho Jumanne Januari 18, 2022.

Share To:

Post A Comment: