Nteghenjwa Hosseah, Shinyanga


Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesema Serikali itapeleka mtambo wa kufia Oksjeni( Oxygen plant) katika Manispaa ya Shinyanga ili kuwapunguzia adha wanayoipata wananchi wa eneo hilo.


Akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani humo amesema kumekuwa na uhitaji wa muda mrefu huduma hiyo kwa wakazi wa Manispaa hiyo  na mahitaji hayo yaliongezeka mara dufu wakati wa wimbi  la ugonjwa wa Uviko-19.


Kutokana na hali hiyo, Dkt.Magembe amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kununua mtambo huo utakaokuwa unazalisha mitungi 200 kwa saa 24 ambao sio tu utasaidia wananchi wa Shinyanga Manispaa lakini pia utasaidia maeneo ya jirani.


Naye, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Yasinta Mboneko amesema wakati wa wimbi kali la ugonjwa wa Uviko-19 walikuwa wanatuma Gari kwenda Mwanza kuchukua Oksjeni na lilikuwa na uwezo wa kubeba mitungi nane tu kwa tripu ilihali mitungi hiyo ilikuwa haiwezi hata kutosheleza mgonjwa mmoja kwa siku.


"Tulikuwa tunapata changamoto kubwa sana Gari linalala barabarani kwa sababu likishusha mitungi nane linarudi saa hiyo hiyo Mwanza kufuata mingine na inakua hivyo kwa saa 24..." 


"Tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia Mtambo wa kuzalisha Oxygeni kwa ajili ya wagonjwa watakaokuwa na uhitaji sasa itakuwepo ya kutosha,"amesema.

Share To:

Post A Comment: