MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila akiwa kwenye moja ya madarasa mapya 26 ya watoto wa awali shule za Msingi Shikizi Muleba 
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila akiwa kwenye moja ya madarasa mapya 26 ya watoto wa awali shule za Msingi Shikizi Muleba 
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila kushoto akiwa kwenye madarasa mapya ya watoto wa awali  shule za Msingi Shikizi Muleba  ambayo 
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila  kushoto akiwa kwenye darasa shikizi la awali shule za msingi Muleba la awali kabla ujenzi wa madarasa mapya 26 ambayo yamewasaidia wanafunzi kukaa kwenye madarasa mazuri yenye ubora
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila  akitazama mmoja ya madaftari ya watoto wanaosoma kwenye shule Shikizi 
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila  akizungumza na wazazi wa watoto ambao wamejitokeza kuandikishwa kwenye madarasa shikizi
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila  kushoto akiwa kwenye darasa la awali shikizi la zamani ambalo kwa sasa halitumiki baada ya ujenzi wa madarasa 26 mapya


NA MWANDISHI WETU,KAGERA

 

 

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera Elias Mahwago Kayandabila amesema halmashauri hiyo imepokea sh.Milioni 520,000,000 ya kujenga vyumba vya madarasa 26 huku watoto wa awali 19,634 wanatarajiwa kusajiliwa kwa mwaka 2022.

 

Akizungumza leo wakati akizungumza kuhusu namna walivyojiandaa ambapo ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 100 kwenye shule 7 zilizopokea fedha hizo na sasa watoto wameanza masomo huku wengine wakiendelea kusajiliwa kwa mujibu wa ratiba ya ufunguzi wa shule hapa nchini.

 

Alisema katika Shule za msingi shikizi zilizopokea fedha na idadi ya vyumba vya madarasa ni pamoja na Daraja Nane (Tsh. 80,000,000 vyumba 4) Kata ya Kimwani, Kashenye (Tsh. 40,000,000 vyumba 2) Kata ya Kagoma,

 

Alizitaja kata nyengine kuwa ni Kyobuheke (Tsh. 40,000,000 vyumba 2) Kata ya Rutoro, Mashekuro (Tsh. 140,000,000 vyumba 7) Kata ya Kasharunga, Mahigabili (Tsh. 140,000,000 vyumba 7) .

 

Mkurugenzi huyo alisema kata nyengine kuwa ni Burungura, Mashasha (Tsh. 40,000,000 vyumba 2) Kata ya Kikuku, Kisha (Tsh. 40,000,000 vyumba 2) Kata ya Bumbile. 

 

Hata hivyo alisema hadi kufikia Januari 17 mwaka  2022 watoto wa shule za Awali takribani 13,000 walikuwa wamesajiliwa.

 

Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: