Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalisti Lazaro ameendesha harambee ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi wilayani humo .


Akizungumza mara baada ya harambee amesema lengo la kufanya hivyo nikutokana na kuchakaa kwa nyumba hizo zilizojengwa mwaka 1919 na baadhi ya Askari kukaa katika nyumba zilizo jengwa na mabanzi.


Amesema lengo lingine la kufanya harambee hiyo ni kuunga 

Mkono juhudi za serikali na Rais Samia ambaye ameshatoa sh.Million 417 000 kwaajili ya kujenga jengo la Utawala wa kituo hicho kilichojengwa na wa koroni na Cha Kwanza hapa Tanzania.


Katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara wadogo na wakubwa ,Wakuu wa Taasisi za serikali na binafsi pamoja na viongozi wa dini jumla sh Milion 42 zilichangwa ikiwemo mifuko ya cement 1230 na mchanga roli 14

Share To:

Post A Comment: