Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu, akishiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Kisiriri kilichopo wilayani Iramba mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya leo wilayani humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu (kulia), akikagua ujenzi wa moja la  darasa ya Uviko 19  kati ya 10 la Sekondari ya Kinambewe wakati wa ziara hiyo.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Iramba, Evance Kibona akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu kuhusu ujenzi wa barabara ya Shelui-Tintigulu yenye urefu wa kilomita 7.3 katika Kata ya Shelui.
Waziri Ummy Mwalimu akikagua ujenzi wa barabara ya Shelui-Tintigulu yenye urefu wa kilomita 7.3 katika Kata ya Shelui. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Iramba,Michael Matomora.
Waziri Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye ziara hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Iramba katika ziara hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na wananchi wa Kata ya Kisiriri wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha kata hiyo.
Ili ni eneo la mto Kinshoka ambapo pata jengwa daraja katika barabara ya kutoka Shelui kwenda Tintigulu.
Muonekano wa darasa la Uviko 19 la Sekondari ya Kinambewe likiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu, akienda kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Kisiriri. Kulia ni Diwani wa kata hiyo, Paul Lyanga na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo.
Afisa Mipango Miji wa Wilaya ya Iramba, Valerian Msigala (kushoto), akitoa taarifa ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu (kulia) ambapo alisema kupitia mradi huo tayari wamekwisha pima viwanja 1,000. 


 Na Dotto Mwaibale, Iramba Singida


SERIKALI imetoa Sh.524,448,800 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Shelui-Tintigulu yenye urefu wa kilomita 7.3 katika Kata ya Shelui wilayani Iramba mkoani Singiga.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Iramba, Evance Kibona wakati akitoa taarifa mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya wilayani humo leo.

Kibona alisema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za tozo kutoka Serikali Kuu na ujenzi wa barabara hiyo unafanywa na Kampuni ya M/s Jp Traders Limited ya jijini Dar es Salaam na kuwa ujenzi huo ulianza rasmi Desemba 11, 2021 na unakadiriwa kukamilika Juni 10 mwakani.

"Mradi huu umelenga kufungua barabara ambapo ujenzi wa kivuko kwenye mto Kinshoka utazingatiwa awamu nyingine kadri bajeti itakavyoruhusu" alisema Kibona.

Kibona alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia sana kufungua mawasiliano na hivyo kurahisisha usafiri katika shughuli za kiuchumi na kijamii kati ya vijiji 6 vya Nselembwe, Tintigulu, Wembere, Kibigiri, Ntwike na Shelui vya Kata ya Shelui na Ntwike vyenye jumla ya wakazi 14,933.

Alisema vijiji vyenye wakazi hao vinajishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji.

Kibona alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo mradi huo ni sehemu ya ongezeko hilo.

Waziri Ummy Mwalimu baada ya kupokea taarifa hiyo aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kuomba fedha mwaka wa fedha 2021/2023 Serikali Kuu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja la Kinshoka ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Mkazi wa Kijiji hicho Neema Mathayo aliishukuru Serikali kwa kuwajengea barabara hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto kubwa ya kupata usafiri wa kwenda kwenye shughuli zao za kiuchumi hasa wanawake wakati wa kwenda Hositali kwa ajili ya kujifungua.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alikagua barabara hiyo, ujenzi wa madarasa kupitia fedha za Uviko 19, mradi wa ujasiriamali wa Wasichana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Kisiriri ambapo pia alizungunguza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: