Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Murtaza Giga, mapema leo ametembelea ofisi za Uhondo Media zilizopo Jijini Dodoma na kujionea namna kazi za kuhabarisha zinavyofanyika.


Pamoja na mambo mengine, Mhe. Giga ambaye ameonesha weledi mkubwa katika kuendesha vikao vya Bunge, tagu la lile la 11 na sasa la 12, amefanya mahojiano maalum na Uhondo TV na kusisiza umuhimu wa vyama vya upinzani nchini kufuata kanuni na miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa sheria.


“Suala la demokrasia ya vyama vingi halikwepeki, demokrasia ina uwanja mpana sana, vyama vingi sio uadui bali ni mawazo mbadala ambayo Serikali inaweza kupokea kwa namna ambayo ni sahihi, lakini utaratibu ufuatwe, kanuni na miongozo ya Nchi na sio kufanya mambo kwa nguvu na mabavu, hakutakuwa na mafanikio kwa namna yoyote”


Pamoja na hayo, Najma Giga amezungumzia mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kama mwanamke wa kwanza kuliongoza Taifa kwa weledi mkubwa.


“Rais wetu amekuwa hodari siku zote, ninamuamini mno kutokana na uzoefu wake kiuongozi, ameanzia mbali tangu Mbunge, baadae Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano kisha akawa Makamu Mwenyekiti wa lile Bunge Maalum la Katiba baadae Makamu wa Rais na sasa kwa mujibu wa Katiba yetu ni Rais wa Tanzania, anao uzoefu na anaweza kwelikweli, ameonesha uwezo huo tumuunge mkono.”-Najma Giga

Share To:

Post A Comment: