Na John Walter-Babati

Zaidi ya nyumba 62 za Kijiji cha Imbilili halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara zimeezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo na kusababisha familia hizo kukosa makazi.

 Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya waathirika, wamesema mvua hiyo ilinyesha kwa takribani saa moja siku ya jumapili Desemba 19,2021 mwendo wa saa 1 Usiku .

Mwenyekiti wa kijiji cha Imbilili Marcel Crisent amesema baadhi ya wananchi hawana pa kuishi tangu jana baada ya nyumba zaidi ya 62 kuezuliwa na upepo huku miundo mbinu ya Umeme ikiharibiwa na miti kuanguka na kwamba wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Mhandisi wa Halmashauri ya mji wa Babati Franko Kapinga akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri amesema kwa sasa wanendelea kufanya tathmini za athari zilizojitokeza kwenye taasisi za Umma na makazi ya watu.

Share To:

Post A Comment: