Na,Jusline Marco:Arusha


Katika kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani,halmashauri ya Jiji la Arusha imeadhimisha siku hiyo katika viwanja vya shule ya Msingi ya Arusha kwa kukutanisha watoto wenye ulemavu kutoka shule mbalimbali ikiwemo shule ya msinhi Meru,Jaffery,Uhuru, Kaloleni pamoja na Themi Sekondari.


Siku hiyo ambayo inatokana na uamuzi wa umoja wa mataifa kutangaza kuwa ni siku ya watu wenye ulemavu Duniani kufuatia azimio namba 47/3 la mwaka 1992 ambapo Tanzania kama nchi wanachama imeridhia na kusaini mkataba na kuadhimisha siku hiyo.


Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha DktJohn Pima,Afisa Elimu Msingi Jiji la Arusha Reginald Richard ameitaka jamii kutotumia watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujipatia kipato.


"Niwashukuru walimu hawa ambao wanawahudumia watoto kwani kutoka kwao tunaweza kupata viongozi na wataalam mbalimbali,hata halmashauri ya jini tuna maafisa Tehama ambao wametoka katika kundi hilihili kwa hiyo tunategemea kupata wahasibu wazuri na walimu wazuri kutoka kwenye kundi holi hili."alisema Afisa elimu huyo


Aidha amesema lengo la maadhimisho hayo ni ili kuihamasisha jamii,serikali na wadau mbalimbali kutambua uwezo wa watu wenye ulemavu na kujenga mazingira yanayotoa fursa ya ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.


Richard amesema kuwa katika Jiji la Aruasha kwa mwaka 2021 halmashauri imeweza kutambua watu wenye ulemavu 1000 kati yao 440 wakiwa ni wanawake na 569 wakiwa ni wanaume ambao wamegawanyika katika makundi tofauti ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu wa viungo 646,ulemavu wa ngozi 77,ulemavu wa kutoona 32,uziwi 84,ulemavu wa akili 156 pamoja na watu ulemavu wa uti wa mgogo 14.


"Ni matumaini yangu wote mnafahamu mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya taifa letu."Alisisitiza Afisa elimu Richard


Aidha amesema katika kipindi cha mwaka 2021/22 vikundi 8 vyenye watu 12 vimepatiwa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 41.2 fedha zilizotokana na asilimia 2 ya mapato ya ndani ambapo pia watu wenye ulemavu wapatao 100 kutoka kwenye Kata zote 25 walipatiwa viti mwendo vyenye thamani ya shilingi Milioni 40 kwa nwaka 2020/21.


Pia Richard ameeleza kuwa jumla ya watu wenye ulemavu 100 walilipiwa bima za afya zinaziwawezesha kupata huduma kutoka katika vituo vya afya katika mwaka huo ambapo wakalimani 3 wa kutafsiri lugha ya alama kwa watu wenye ulemavu wa uziwi wameajiriwa na halmashauri.


Ameongeza kuwa yapo mafanikio mbalimbali yaliuopatikana katika kipindi cha mwaka 2020/21 kuwa ni pamoja na kuwepo kwa madarasa rekebishi ndani ya vitengo kupitia mpango wa mtu binafsi kujifunza kulkngana na mahitaji yake pamoja na kutumia mifumo ya serikali ili kupata taarifa sahihi zs wanafinzi wenye ulemavu zitakazo wezesha kuandaa vifaa kulingana na mahitaji yao.


Vilevile ameeleza kuwa mafanikio mengine ni uwepo wa miundombinu rafiki kwenye vitengo kulingana na uhitaji wa aina ya ulemavu,serikali kupata ushirikiano wa asasi zilizo onyesha utayari wa kuandaa mazingira ya kuajiriwa na kujiajiri kwa watu wenye ulemavu katika nyanja za kushona,kupika,kupamba na kuchora.


Ameeleza kuwa watu wenye ulemavu wapatao 418 walipatiwa huduma ws msaada wa kisaikolojia pamoja na misaada mingine ikiwemo kofia ya jua,mafuta maalum,vifaa vya kusomea huduma ya kutembelewa na madaktari wa ngozi na macho kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu 233 wamefikiwa na kupatiwa elimu ya UVIKO 19.


Vilevile alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya wimbi la 4 la ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kuendelea kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ambapo ameomba kutumika kwa vifaa vyote muhimu vya kujikinga na ugonjwa huo kutumika majumbani.


Sambamba na hayo pia amewaomba wananchi kujitokeza kuwaandikisha darasa la kwanxa watoto wote pamoja na wale wenye mahitaji maalum ambao wamefikia umri kwa kwenda shule,eapelekwe kwani nao wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.


Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Chama cha Watu wenye Ulemavu Jiji la Arusha Emmanuel Benjamin amesema kuwa pamoja na maadhimisho hayo bado zipo changamoto mbalimbali zinazowakabili kama walemavu kuwa ni pamoja na miundombinu isiyokuwa rafiki katika maeneo ya kutolea huduma,mawasiliano magumu kati ya watu wenye ulemavu.


Ameengeza kuwa changamoto nyingine ni upungufu wa thamani kwa wate wenye uhitaji,jamii kuwaficha watu wenye ulemavu majimbani na kutowapeleka kupata elimu na huduma mbalimbali pamoja na  tatizo la ajira japo kuwa wstu wenye ulemavu wana ujuzi katika fani mbalimbali.


Pamoja na changamoto hizo kama watu wenye ulemavu wametoa mapendekezo yao ambapo wsmeomba kujengwakwa miundombinu  rafiki kwenye taasisi za serikali na taasisi binafsi hasa katika majengo mapya yanayojengwa,somo la lugha ya alama lifundishwe kwa jamii yote na walemavu kupewa kipaumbele katika ajira ikiwemo wale wsnaojifunza ujasiriamali kupewa eneo ambalo litawezesha kuonekana kwa vitu wavyo  vitengeneza na kununulika.


Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Jiji la Arusha Bi.Mary Shisaeli Mwasha amewapongeza walimu ambao wametumia muda wao kuwafundisha wanafunzi hao na kuwafanya kuwa na bidii katika kazi walizofundishwa.

Share To:

Post A Comment: