Na John Walter-Hanang


Kuelekea wiki ya nenda kwa Usalama barabarani, jeshi la polisi Kikosi cha cha usalama Barabarani wilayani Hanang mkoani Manyara Novemba 3,2021 limetoa mafunzo kwa madereva wa Bajaji na Maguta wakilenga kupunguza vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu kupitia vyombo hivyo.

Akifungua mafunzo hayo mkuu wa Polisi wa wilayani hapo Mratibu mwandamizi wa Jeshi la polisi (SSP) Sweetbert Kisha, amesema kuwa mara nyingi abiria wanalalamika kuibiwa mizigo yao pamoja na fedha pindi wakiwa kwenye usafiri hivyo ametoa rai kwa madereva wote kutoa taarifa pindi wanapopata taarifa za wizi na ikiwezekana wamkamate muhusika na kumfikisha kwenye vyombo vya dola.

Amesema wapo baadhi ya madereva wa vyombo hivyo vya moto kwa kukosa uaminifu hushiriki kubeba mizigo kuwa ni rahisi ya wizi kwa tamaa ya kupata pesa jambo linalochafua taswira nzima ya kazi hiyo na kuonekana ya hovyo.

Amesema pamoja na kutii sheria za usalama barabarani,ni jukumu la kila mmoja kudhibiti wizi wa pikipiki na wizi wa aina nyingine.

Aidha aliwataka madereva waifanye Kazi hiyo kwa kuzingatia maadili na kuwafichua wanaofanya vitendo vya uhalifu kwa kutumia vyombo hivyo vya moto.

Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani hapo Volca Willa amesema kuwa katika wiki hii ya nenda kwa usalama barabarani kikosi cha usalama wilayani hapo kimeamua kutoa elimu hiyo ili kuwakumbusha madereva majukumu yao pindi wakiwa katika shughuli za kujipatia kipato.

Willa amewasisitiza madereva hao kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazochangia kuangamiza maisha ya watu huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.

Willa amesema wataendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya madereva wilayani humo ili waendelee kuwa salama wao pamoja na abiria wanaowabeba na kwamba kwa atakaekwenda kinyume na hapo watamuajibisha kisheria.

Madereva waliohudhuria semina hiyo wamelihakikishia jeshi la polisi kutoa ushirikiano wa pindi linapotokea tukio la uhalifu hasa kwa abiria huku wakibainisha kuwa wanaofanya matukio ya aina hiyo ni wale wanaovamia kazi ya udereva kwa lengo la kuiba.Maadhimisho ya siku ya nenda kwa Usalama barabarani ,yanatarajiwa kufanyika Novemba 11-20,2021 ambapo yanatajwa kitaifa yatakuwa katika viwanja vya shekh Amri Abeid Jijini Arusha yakibebwa na kauli mbiu isemayo ''Jali maisha yako na ya wengine
Share To:

Post A Comment: