Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo


WAZIRI ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri nchini,kuacha kuwabania ruksa walimu kwenda kujiendeleza kimasomo na kuhakikisha wanatenga bajeti katika raslimali watu katika kuwaendeleza kielemu ili kuleta mabadiliko chanya.

Ummy aliyasema hayo katika mahafali ya 29 ya chuo Cha Wakala wa maendeleo ya elimu (ADEM ) Bagamoyo,Pwani kwa wahitimu wa stashahada ya uongozi na usimamizi wa elimu-DEMA,stashahada ya ukaguzi wa shule na astashahada ya uongozi, usimamizi na utawala katika elimu.

Amewaelekeza wakurugenzi wa Halmashauri kutoa fursa kwa walimu kwenda kujiongezea elimu ,"tumesomewa taarifa ya chuo kati ya walimu 1,345 walitakiwa kupokelewa kwenda kusoma walimu 408 hawakuripoti kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa ruksa.

Ummy alieleza ,atahakikisha katika bajeti ya mwaka mpya wa fedha ya mwaka 2022/2023 Halmashauri zinatengewa fedha kwa ajili ya raslimali watu katika kuwaendeleza kielemu ili kuleta mabadiliko chanya katika suala la elimu mashuleni.

Alisema ,hatua iliyopo Sasa ni muda wa kuandaa bajeti hiyo Lakini ifikapo mwakani anaamini Halmashauri zitakuwa na bajeti kwa ajili ya kuwasomesha watumishi hao.

Ummy amefurahi kusikia wahitimu hao wamekwiva katika masomo ya uongozi, usimamizi wa elimu-DEMA,utawala na masuala ya takwimu na amewaahidi kutoa kipaombele kwao kuweza kuteuliwa nafasi za uongozi kulingana na sifa walizopata.

"Eneo hili tumeshuhudia baadhi ya Halmashauri zikiwa zinateua nafasi hizo kwa kupendelea watu wasio na sifa kwenye nafasi ya ualimu mkuu na maafisa elimu kata."alisisitiza Ummy.

Ummy alibainisha Serikali ya awamu ya sita imetenga Bilioni 150 kwa ajili ya elimu bila malipo.

"Tumeshuhudia fedha hizi zikiwa zinapanda ,katika Serikali ya Samia Suluhu Hassan kutoka bajeti ya sh.bilioni 20.8 hadi Bilioni 26 na Sasa kufikia Bilioni 150"

Pamoja na Hilo, Ummy Rais Samia ametoa kiasi cha sh.bilioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 12,000 na atahakikisha anasimamia yakamilishwe kwa wakati.

Mtendaji mkuu ADEM Dkt.Siston Mgullah alifafanua,Mhitimu Philbert Nyanda akisoma taarifa ya wahitimu alisema, walimu wanapata changamoto ya kunyimwa ruksa ya kujiendeleza kimasomo kutoka kwenye Halmashauri zao Pamoja na kushindwa kupandishwa madaraja kwa kisingizio Cha kwenda kusoma.

Aliomba utaratibu huo uangaliwe kwani unashusha nguvu kwa walimu kwenda kujiendeleza kimasomo.



Share To:

Post A Comment: