Na Asila Twaha, Morogoro


Timu ya mpira wa miguu ya TAMISEMI imetwaa ubingwa wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali SHIMIWI ikiifunga timu ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa magoli 7 - 0.


Mchezo wa fainali umechezwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro Novemba 02, 2021 mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa alifika uwanjani hapo kwa ajili ya kufunga mashindano hayo.


Katika kipindi cha kwanza TAMISEMI walikua wameshailaza timu ya Katiba na Sheria kwa magoli 3 – 0 lakini hayo hayakutosha baada ya kuingia kipindi cha pili waliumiliki mchezo na kuongeza magoli mengine 4.


Katika mashindo hayo TAMISEMI Sports Club imeweza kutoa ubingwa katika michezo mbalimbali ikiwemo mchezo ya drafti ambapo mchezaji Salum Simba aliyemshinda mpinzani wake kutoka Maliasili katika mchezo wa fainali kwa alama 2 – 0.


Kwa upande wa mchezo wa riadha TAMISEMI iliibuka mshindi katika mita 100, 1500 na 800 kwa wanaume na wanawake mita 100, 400, 800 na 1500.


Mchezo wa kamba kwa wanawake TAMISEMI hawakuwa nyuma kwani walifanikiwa kushika nafasi ya tatu.


Mashindano hayo yalianza Oktoba 20, 2021 na kuzinduliwa rasmi Oktoba 23, 2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na kufungwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa Novemba 02, 2021.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: