Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki ametoa wito kwa Wakala wa Vyuo vya mafunzo ya mifugo (LITA) kuongeza wigo wa utoaji Mafunzo kwa wafugali ili wawe na mtizamo wa  kufuga  kisasa na kupata  faida zaidi.


Mhe. Ndaki amesema hayo alipotembelea LITA kampasi ya  Tengeru,Wilayani Arumeru  ambayo ni miongoni mwa kampasi nane nchin, ambapo  ameihimiza LITA mbali na kutoa Mafunzo kwa Wanafunzi, iweke pia mazingira rafiki na rahisi ya  utoaji  elimu  kwa wafugaji ili waelewe na kufanya ufugaji  wa kisasa  wenye tija kwa mfugaji  na katika  uchumi wa Taifa"ufugaji unaenda pamoja na malisho hivyo LITA tumieni mashamba darasa yenu kuwaelimisha wafugaji upandaji wa malisho ya mifugo yao "amehimiza Mhe.Ndaki


Vilevile Mhe.Ndaki ametoa wito kwa LITA kuwajenga  wanafunzi wa Vyuo vya mifugo  katika misingi ya  kujiajiri pindi watakapo hitimu ili kuwa na wafugaji wenye ujuzi katika jamii ambao  watahamasisha ufugaji wa kisasa  na Wenye tija zaidi


Naye, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi, Richard Ruyango amepongeza LITA Tengeru kwa kutumia mapato yake ya ndani kuboresha miundombinu , ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike iliogharimu Milioni 166.3 ambayo imezinduliwa na Mhe.Waziri Ndaki"kipekee niwapongeze Sana LITA Tengeru kuongeza mapato yake ya ndani kutoka Bilioni 3 hivi hadi kufikia zaidi ya Bilioni 4 "amesema Ruyango


Meneja wa LITA Tengeru Janeth Bendera amesema mbali na mafanikio makubwa ya kuwa na ongezeko la wanafunzi wanaojiumga na LITA Kampasi ya Tengeru  kutoka 657 mwaka 2018/2019 hadi 1,579 Mwaka 2020/2021 Kuna upungufu wa  miundombinu  na mingi ni chakavu .


Aidha Mhe.Ndaki mbali na kuzindua hosteli ya wanafunzi 80 wa kike , ametembelea ujenzi wa vyumba vya Madarasa ,ukarabati  mkubwa wa Maabara mbili za parasatioloji na multipurpose pamoja na eneo la upandaji malisho ya mifugo.

Share To:

Post A Comment: