NA HERI SHABANI


MKURUGENZI wa WAHENGA Aluminiaum Tanzania John Ryoba Mrema, amelishauri Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutunga sheria kwa ajili viongozi wanaochaguliwa na Wananchi wapewe adhabu kwa kutoa ahadi hewa kwa wapiga kura wake.


John Ryoba Mrema alisema hayo Dar es Salaam jana katika Mahafali ya12  kidato cha nne Shule ya Sekondari ALI iliyopo Kinyerezi.


" Nalishauri Bunge letu tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutunga sheria ndogo ya kuwabana Viongozi wetu ambao wanachaguliwa na wananchi kwa kutoa ahadi alafu kushindwa kuzitekeleza "alisema Ryoba .


Alisema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipitisha sheria hiyo itasaidia kuwahimiza kutekeleza kwa wakati   zile ahadi zao wanazotoa kwa wananchi.


Wakati huohuo alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha  kusaidia sekta ya Elimu Wilaya ya Ilala kwa ajili ya ujenzi wa madarasa shule za Sekondari pamoja na miradi ya maendeleo


Amewataka Watanzania kumsaidia Rais katika Tanzania ya Uchumi wa Viwanda kutoka uchumi wa kati kwenda uchumi wa kwanza.


Akizungumzia shule ya Sekondari ALI alisema atashirikiana na Serikali katika kusaidia kutatua changamoto za shule hiyo ili iweze kufikia malengo yake  ikiwemo  kuboresha miundombinu .


Aliwataka Wazazi kuwasimamia watoto waweze kutimiza ndoto zao katika sekta ya elimu kuanzia elimu ya Msingi sekondari hadi chuo kikuu


Kwa upande mwingine alisema kumaliza kidato cha nne sio mwisho wa elimu atasaidia  kulipa  ada ya masomo wanafunzi wawili wa shule hiyo ambao wamehitimu.Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ALI Frola Msonge, alisema shule ilianza mwaka 2007 jumla ya wanafunzi waliomaliza 400.


Mwalimu Frola Msonge alielezea mafaniko ya shule yake kwa kipindi cha miaka minne alisema shule hiyo wameongezeka walimu wa Sayansi na Sanaa ,kujengwa kwa mahabara za kisasa kwa ajili ya masomo kwa vitendo,mikakati ya Walimu ,Wazazi na wanafunzi katika kujenga taaluma ,Pia alimpongeza  Mjumbe wa Viti Maalum Mtaa wa Kanga  Nura Yusuph Matona, kuwaunganishia maji DAWASA  bomba la shule.


Akielezea changamoto za shule yake Kisima cha shule chakavu miondombinu yake ,changamoto zingine Photocopy mashine ,Printer na Laptop.

Share To:

Post A Comment: