SKatika Mkutano Maalamu wa Tawi la Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Makuti “B”, Kata ya Magomeni, Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam na uzinduzi wa Programu maalum ya Tawi hilo iitwayo _”RAIS WETU, SHUJAA WETU”_  Komred Abrahman Abdalah Kassim Mwenyekiti wa Tawi hilo, ametoa rai kwa Vijana Nchi nzima kumuunga Mkono Mhe. Samia Suluhu Hassani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Akieleza suala hilo kwa undani Kamaradi Abrahman amesema Mhe. Samia anafanyakazi kubwa sana ya ubunifu na udhubutu kwa manufaa ya Wananchi na haswa Vijana kwenye sekta zote zikiwemo Uchukizi, Afya, Kilimo, Umeme, Utalii na Uwekezaji, hivyo ni muhimu Vijana Nchi nzima wanaoipenda Tanzania kumuunga Mkono. 


Wakati uo huo Tawi la Makuti “B” limeendesha Kongamano kubwa la lenye mada itwayo _NAFASI YA TAWI KATIKA UJENZI WA CHAMA NA TAIFA_  lililoongozwa na  mgeni rasmi Ndugu Laila Baruan Ngozi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM. 


Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa ngazi ya Tawi hadi Taifa, ambapo Vijana wamejishehenesha na maarifa na taarifa sahihi za Ujenzi wa Chama na Taifa. 


Huu ni muendelezo wa kazi za Jumuia ya Vijana Tawi, kwa maslahi mapana ya Vijana. 


Imetolewa na

Katibu Hamasa wa Tawi 

Makuti B

Share To:

Post A Comment: