Na Lucas Myovela_ ARUSHA
Naibu waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande akikagua moja ya mabwawa ya maji taka katika kiwanda cha Raha Beverages kilichopo Jijini Arusha.


Serikali imewataka wenye viwanda hapa nchini kuhakikisha wanaweka mifumo sahihi na ya kisasa  kudhibiti Maji taka yanayotoka kiwandani na kuacha kuyaelekeza kwenye makazi ya wananchi  hatua itakayo saidia kuondoa uharibifu wa mazingira na kuleta madhara ya kiafya Kwa binadamu.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande wakati alipotembelea kiwanda Cha TBL ,Raha Beverages , Fiberboard na bwawa la kisasa la Maji taka la Auwsa ,katika ziara iliyolenga kuangalia utekelezaji wa Sheria na kanuni za mazingira katika jiji la Arusha.

Naibu waziri akiwa ameambatana na viongozi wa NEMC Mkoani hapa,aliridhishwa na mfumo wa kudhibiti Maji taka unaotumiwa na kiwanda Cha TBL na kampuni ya Raha beverages wa kuchakata na kuyarejesha upya kiwandani Kwa ajiri na matumizi mengine jambo ambalo amevitaka viwanda vingine kuiga mfumo huo.
Akiongea mara baada ya kutembelea kiwanda Cha Raha beverage na kukagua mtambo wa kuchakata Maji taka,naibu waziri alikipongeza kiwanda hicho Kwa ufanisi wa kudhibiti Maji taka kutoenda kwenye makazi ya Watu na kuvitaka viwanda vingine kujifunza kutoka kampuni hiyo ya Raha.

Hata hivyo alisema ipo dhana Kwa baadhi ya viwanda kutiririsha Maji taka ya viwandani kwenye makazi ya Watu Kwa madai kwamba Maji hayo yamechakatwa na hayana madhara Kwa binadamu na mimea ila tunafanya mpango kwa kutuma wataalamu wetu ili kujiridhisha .

"Tutatuma wataalamu wetu kwenye viwanda vinavyotiririsha Maji kwenye makazi ya watu  wakidai Maji hayo  hayana madhara ili wafanye uchunguzi na Serikali itatoa tamko, yapo malalamiko mengi ya wananchi yanayohitaji majibu ya wataalamu"alisema Naibu Waziri.

Kwa upande wake meneja wa mauzo na masoko katika kiwanda Cha Raha Beverages , Daniel Olomi alimweleza naibu waziri kwamba  kiwanda hicho kinachotengeneza mvinyo aina ya Raha ,kinatumia mfumo wa kisasa wa kudhibiti  Maji taka yanayotoka kiwandani ili kuweza kutumika Kwa matumizi mengine bila kuleta madhara.

"Tumekuwa ni wadau wazuri wa kutunza Mazingira hasa kwa nanchi wanao tuzunguka, Pia tumekuwa wadau wazuri wa ulipaji wa kodi ya Serikali kwa kutumifumo mpya na katika hili tunawakaribisha viongozi wengina hata Mhe, Rais Afike hapa ajionee jinzi tulivyo wadau wazuri kwa Serikali yetu katika swqla la maendeleo kwa ulioaji kodi". Ameeleza Daniel Olomi.
"Na pia nitoe wito kwa nanchi ambao ni wateja wa vinywaji vyetu kuangalia kwa makini katika kuangalia stika zetu za kodi ili kuepusha watu wanaoiga vyiwaji vyetu maana sisi kila kinywaji kina stika yake ya kodi haya yote ni kwaajili ya uzalendo dhidi ya Nchini yetu". Aliongeza Daniel Olomi.

Aidha Daniel alieleza kwamba Kampuni ya Raha Bereveges Kwa muda mrefu imekuwa ikitumia mfumo huo wa kisasa wa kusafisha Maji taka ya kiwandani ili kuweza kutumika Kwa ajili ya umwagiliaji wa mimea Bila kuwa na madhara .


Katika hatua nyingine naibu waziri alitoa maagizo Kwa kiwanda Cha kutengeneza mbao Cha Fiberboard kilichopo Njiro ,jijini hapa kuhakikisha kinaondokana na matumizi ya nishati ya Kuni badala yake kijikite kwenye matumizi ya nishati mbadala ambayo ni rafiki wa mazingira na binadamu kwa ujumla.

Kwa upande wake Meneja wa TBL  Arusha Bw, Joseph Mwaikasu ameeleza kuwa kwa mashirikiano waliyo nayo na wananchi jirani juu ya utunzaji wa mazingira wameweka miundo mbinu rafiki ya maji taka na kwa kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wanao ishi maeneo jirani na kiwanda hicho cha TBL. Jijini Arusha.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: