Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Salehe Mkwizu leo amefanya Ziara ya kimsingi ya kikatiba ya kutembelea miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika wilaya ya rombo.


Mkwizu amesema fursa pekee katika mazingira baadhi yenye Misitu kufuga nyuki ni rafiki kwani inawezesha jamii kujipatia kipato na kuacha kufanya Biashara ambazo zitawapatia hasara kubwa na kushindwa kuendeleza kazi zao.


"Na kama msitu upo sehemu kama hii na wanaruhusu watu kufuga nyuki basi Halmashauri zetu ziweze kuwawezesha wale wananchi kufuga nyuki na kujipatia kipato kuliko wengine wanaoenda kuhangaika na biashara ambazo hawazifahamu na mwisho wa siku wanashindwa kurejesha zile fedha na fedha hizo zinashindwa kurudi kuwasaidia wananchi wenye uhitaji.,"amesema Mkwizu

Mkwizu ametoa wito kwa Tarura wahakikishe wanashirikiana na baraza la madiwani kwakuwa madiwani ndiyo wanajua barabara zenye vipaumbele.


"Kubwa ambalo nimezungumza leo ni kwamba tumewaagiza ndugu zetu wa Tarura wanapokuja kutekeleza miradi ya maendeleo ya barabara wahakikishe wanawashirikisha madiwani kwakuwa madiwani ndio wanaojua barabara zenye vipaumbele , wanajua barabara gani zina changamoto." Mkwizu


Hata hivyo Mkwizu ametoa shukrani zake za pongezi kwa Halmashauri ya wilaya ya Rombo kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya pia ametoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita ambayo imetoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali kama ujenzi wa hosptali mpya ya Wilaya ya Rombo, ujenzi wa madarasa pamoja na barabara.

Share To:

Post A Comment: