Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Maziwa cha  Taish Farm kilichopo Kijiji cha Mtipa Mtaa wa Mwembemmoja Manispaa ya Singida, Hassani Tati akitoa taarifa ya kiwanda hicho kwa Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge alipotembelea kiwanda hicho jana.

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge akiangalia maziwa yanayozalishwa katika kiwanda hicho.

Meneza Uzalishaji wa kiwanda hicho Ladislaus Mughai akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati wa ziara hiyo.

Maziwa yanayotengenezwa kiwandani hapo.
Baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye ziara hiyo.
Baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye ziara hiyo.

Muonekano wa kiwanda hicho.


Na Waandishi Wetu, Singida


MKUU wa Mkoa SingidaDkt. Binilith Mahenge amesema Serikali mkoani hapa  itaendelea kuwasimamia na kuwaunga mkono wawekezaji wadogo wa ndani ambao wamewekeza katika sekta tofauti kwa sababu wamekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa na kuongeza ajira kwa watanzania.

Dkt. Mahenge aliyasema hayo jana alipotembelea kiwanda cha maziwa cha muwekezaji mdogo kinachofahamika kwa jina la TAISH Farm kilichopo katika Kijiji chaMtipa Mtaa wa Mwembemmoja Manispaa ya Singida.

Mahenge alisema Serikali itaendelea kutoa mazingira wezeshi kwa wawekezaji ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinzowakabili.

Aidha amempongeza Mkurungezi wa kiwanda hicho Hassani Tati kwa kusaidia upatikanaji wa soko la maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo ambapo hununua lita zaidi ya 70.

Hata hivyo kiwanda hicho kimekuwa kikizalisha ajira kwa wananchi kupitia mnyororo wa thamani ambapo kimeajiri watumishi na wengine kupata ajira katika maduka ya kuuzia maziwa hayo.

Akijibu changamoto za ubovu wa barabara, ukosefu wa umeme zilizotajwa na mkurugrenzi wa kiwanda hicho, Mkuu waMkoa amewaagiza TANROAD naTARURA  kupeleka ofisini kwake mpago wa utengenezaji wa barabara hiyo inayoingia kiwandani hapo ili washauriane na  kuanza utengenezaji mara moja.

Aidha amewataka Tanesco   kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanafikisha umeme katika eneo hilo la kiwanda ikiwa ni pamoja na vijiji vingine 12  vilivyo ndani ya Manispaa ya Singida ili kurahisisha uwekezaji na uboreshwaji wa kiwanda hicho.

Alisema zoezi la upelekaji umeme katika maeneo hayo anaamini litakuwa rahisi kwa kuwa Tanesco wamepewa zaidi ya Sh.Bilioni 3  ili kusambaza  umeme vijijini.

Mahenge amemshauri mwekezaji huyo kuchukua mkopo benki ili aweze kununua mashine zakisasa kwa ajili ya uongezaji wa thamani ya maziwa kwa kuwa Serikali itatua changamoto za barabara pamoja na upatikanaji  wa  umeme wa uhakika.

“Bado unanafasi ya kuongeza uwekezaji na kufanya vizuri zaidi hivyo nakushauri ufungue vituo vidogo vya kukusanyia maziwa ambapo utakuwa unapima ubora huko huko,hii itamsaidia mfugaji kutotembea mwendo mrefu na maziwa yataendelea kuwa salama zaidi”. alisema Mahenge.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho Hassani Tati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa alisema kiwanda hicho kwa muda wa miaka mitano kimekuwa kikitengeneza bidhaa mbalimbali za maziwa zikiwemo mtindi, maziwa fresh na yogati  zenyeladha tofauti.

Alisema maziwa hayo yananunuliwa kwa wafugaji waSingida na yanauzwa Manyoni, Ikungi, Singida mjini, Mkalama, Shelui, Igunga na Dodoma.

Aidha Tati alisema pamoja na changamoto ambazo Serikali itazitatua bado kunachangamoto ya upatikanaji wa vifungashio vya bidhaa hiyo ambapo wanalizimika kuviagiza nje ya nchi.

Tati aliomba Serikali kutafuta wawekezaji wengine wa vifungashio ili kuachana na uagizaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: