Yamesemwa hayo na mwenyekiti  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Mhe. Zelothe Steven alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi za forodha katika kituo  cha mpaka wa Namanga Wilayani Longido.

Serikali inapoteza Mapato mengi kutokana na utoroshaji wa Mifugo katika mpaka huu, hatuko tayari kuona mapato yanaendelea kupotea zaidi.

Wafugaji wanaotaka kusafirisha Mifugo nje ya nchi lazima wafuate sheria, taratibu na kanuni hususani za ulipaji kodi.

Aidha, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Nurdin Babu kubaini mtandao huo unaotorosha Mifugo kwani wanahujumu uchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema Serikali ya awamu ya  sita   imeweka nguvu kubwa katika uwekezaji wa Viwanda, hivyo Serikali ya Mkoa itahakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuweka vivutio vya kuwavutia.

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Nurdin Babu amesema wafugaji hawakatazwi kupeleka Mifugo yao kuuza nje ya nchi bali wanatakiwa watoe ushuru kwa Halmashauri na Serikali kuu.



Share To:

Post A Comment: