Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi 'CCM' Daniel Chongolo akizungumza na wajumbe Secretarieti ya Taifa katika ukumbi wa Kambi ya SGR Kilosa mkoani Morogoro.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameagiza ndani ya siku
14 vongozi wote wa Chama hicho na kamati zao za siasa kuanzia Mkoa na
Wilaya kushuka chini kukagua miradi yote ya maendeleo inayowazunguka.
Chongolo ametoa maagizo hayo leo Agosti 10,2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reri ya kisisasa SGR.
"Niwapongeze
watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonyesha njia nami nimeamka Nije hapa
na secretarieti yangu kujionea je kinachofanyika hapa ni kile
kinachoubiriwa,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na
maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote
tushuke chini kukagua miradi ya Maendeleo katika Maeneo yetu ."
Amesema
wao wanawajibu wa kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani
sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya
Kwa
upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja
Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa
ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa
hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia
sasa.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Martin Shegela
amesema uongozi wa mkoa huo umeridhishwa na kasi ya ujenzi kwani
waliweza kutembelea eneo la kuanzia Kilosa mpaka Morogoro Station.
Amesema
kuwa mradi huo umekuwa kichocheo kikubwa Cha uchumi wa Morogoro kwani
wamekuwa wakitumia malighafi na bidhaa nyingi kutoka mkoa huo.
Mkurungezi wa Shirika la Reli Tanzania,Masanja Kadogosa akitoa neno kwa ujumbe secretarieti ya CCM Taifa inayotembelea mradi wa SGR kuanzia Kilosa kuja Dar es Salaam.
Sehemu ya Daraja linalo katisha mto Mkondoa ambapo Reli ya mwendokasi inapita juuMkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akitoa maelekezo kwa wajumbe wa secretarieti ya Taifa waliofika kukagua ujenzi Reli ya kisasa wa SGR
Post A Comment: