Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Zainab Chaula alipotembelea ofisi za Shirika la Posta na kuangalia namna walivyojiandaa kwa ajili ya huduma ya One stop Centre (Huduma Pamoja Centre) itakayotoa huduma taasisi zote za Kiserikali nchi nzima.

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknlojia Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi mbalimbali wa Kiserikali watakaokuwa wanatoa huduma zao ndani ya ofisi za Shirika La Posta Nchini.

...............................................................

Na.Mwandishi wetu

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) limeanza kutoa Huduma Pamoja Centre kwa taasisi za kiserikali ili kurahisha na kupunguza usumbufu kwa wananchi.

Huduma hiyo iliyoanza kutolewa Julai Mosi mwaka huu inazihusisha taasisi zote za kiserikali za zitatoa huduma zote ndani ya ofisi moja.  

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Zainab Chaula amesema mpango huo ni mkakati wa muda mrefu wa serikali katika kuziunganisha taasisi za kiserikali kufanya kazi kwenye ofisi moja.  

Akizungumza na waandish wa habari baada ya kutembelea ofisi za Shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, Chaula amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi yake kidigitali kwa kuzileta taasisi zote muhimu pamoja ndani ya ofisi moja ambayo nayo ni Shirika la Posta.

  Amesema Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia imeweka mikakati katika kusimamia mifumo ya kidigitali ili kupunguza usumbufu kwa wananchi pindi wanapotaka huduma kwa uharaka zaidi. Chaula amesema amefanya kikao na wakuu wa taasisi zote na kuwataka waongeze muda wa kufanya kazi ili wananchi wengi waweze kupata huduma. 

 Huduma hizo zote zitakuwa zinatolewa ndani ofisi za Posta ambapo kwa sasa imeanza katika mkoa wa Dodoma na Dar es salaam na amezipongeza taasisi zote kwa kuweza kuamua kwa pamoja kuweka ofisi za Posta kwasababu kila siku wanataka huduma na njia rahisi ni kuwasogezea karibu Kaimu Postamasta Mkuu Macrice Mbodo amesema hadi kufikia Septemba mwaka huu watakuwa wamefikia ofisi 10 zitakazokuwa zinatoa huduma hizo.  

Amesema Shirika la Posta lipo nchi nzima na huduma hizo zitakuwa zinapatikana ndani ya ofisi zao zote na kwa hilo itaondoa usumbufu na gharama kwa wananchi. 

Amesema shirika wamejipanga kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi wote Kaimu Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Usajili Vizazi na Vifo RITA Emmy Hudson amesema katika ofisi za Posta watakuwa wanatoa huduma ya vyeti vya kuzaliwa na vifo. 

Amesema kwa sasa ukifika katika ofisi za Posta ndani ya Jiji la Dodoma na Dar es salaam utakuta ofisi zao na huduma zote utazipata na itapunguza usumbufu kwenda ofisi za RITA. Ameishukuru na kuipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa wananchi kupata huduma zote muhimu ndani ya ofisi moja.

  Kwa sasa ndani ya ofisi za shirika la posta litakua linatoa huduma mbalimbali za kitaasisi kama NIDA, BRELA, RITA, NSSF, uhamiaji na zinginezo.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: