Msajili Mwandamizi kutoka RITA, Rehema Mushi akitoa  huduma kwa mwananchi waliofika katika banda hilo leo katika ya maonesho 45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa RITA, Edwin Mbekenga  akitoa huduma kwa Wananchi waliojitokezaa kwenye banda la RITA katika  maonesho 45 ya Biashara ya Kimataifa  ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Barabara ya Kilwa wilaya ya Temeke  mkoa wa  Dar es Salaam.
 
 
WAKALA wa usajili ufilisi na udhamini RITA Ni moja ya Taasisi inayotoa na inaendelea  na huduma katika  maonesho ya 45 ya Sabasaba. Hivyo  Wananchi wananufaika na maonyesho hayo huku wakijitoteza kwa wingi na kuendelea kupata huduma ya vyeti vya kuzaliwa kwa urahisi zaidi mpaka Sasa Wananchi waliojitokezaa na kufanya usajili huo   takribani zaidi ya wnanchi Elufu Moja na zaidi washajiandikisha na watapatiwa vyeti vyao kabla ya maonyesho hayo kuisha, hivyo Wananchi mnakaribishwa kufika kwenye viwanja hivi ili  kupata fursa ya  huduma za RITA   kwa urahisi na Ada yake ikiwa  Ni shilingi 10000 tu, Amesema Msajili Mwandamizi kutoka RITA, Rehema Mushi
Share To:

Post A Comment: