Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David kafulila amewataka wakuu wa wilaya katika mkoa huo kufungua milango ya ushirikiano na jamii ya wafanyabiashara ili kuchochea maendeleo katika Mkoa huo.

Amesema kwa pamoja wanajukumu la kuchangamana katika kuleta maendeleo kwa sababu jamii ya wafanyabiashara inamajibu mengi ya changamoto ambazo zinaweza kukwamisha maendeleo.

Kafulila ameyasema hayo alipokuwa katika hafla ya kumuaga aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Miriam Mbaga iliyofanyika Julai 5, na kuhudhuliwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Simiyu.

"ushirikiano huo utatumika kujenga mawazo mapya katika jamii,Isiwe kwamba mkuu wa wilaya mtu aone kumfikia ni shida, hapana tengenezeni milango ya kufikika ili mkutane mkae na kuzungumza maendeleo", alisema.

Aidha amewataka wafanyabiashara kuendelea kushiriki katika kuinua ubora wa elimu mkoani humo kwa kuichangia sekta ya elimu ili kuendelea kuwapa nafasi zaidi wanafunzi waliopo katika madarasa ya mitihani kufanya vizuri.

Katika hatua nyingine kafulila amewataka wafanyabiashara wa zao la Pamba kushirikikiana na wakulima wa zao hili katika kukifanya kilimo cha pamba kuwa kilimo chenye tija ili kufikia malengo ya mkoa ya kuzalisha pamba tani 500,000.

"Tuzidi kuchanga mawazo, tushirikiane, tumsaidie huyu mkulima tangu hatua za awali ilitija katika shughuli zao iongezeka".
Share To:

Post A Comment: