Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anastazia Tutuba akifungua rasmi mafunzo shirikishi ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu Wilayani same ambapo amewataka wananchi kuwa wakweli katika kutoa taarifa ya matukio ya uvamizi wa wanyamapori katika maeneo yao. Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ambapo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa askari wanyamapori katika kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu. Mtafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa wanyamapori Nchini (TAWIRI), Dkt. Janemary Ntalwila akitoa maelezo ya awali wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo shirikishi mbinu za kudhibiti migongano baina ya wanadamu na wanyamapori waharibifu na wakali,wilayani same mkoani Kilimanjaro.

 Serikali kupitia Wizara ya maliasili na utalii imeendelea kutoka mafunzo shirikishi ya mbinu za kudhibiti migongano kati ya wanyamapori Wakali na waharibifu kwa lengo la kuwalinda wananchi na mali zao. 

Akizungumza Wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa vijiji vya wilaya za Same na Mwanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anastazia Tutuba amesema pamoja na Serikali kuweka nguvu ya katika kupambana na changamoto ya wanyamapori katika maeneo ya makazi ya binadamu, wananchi nao wanapaswa kuwa wakweli katika utoaji wa taarifa za matukio ya uvamizi wa wanyamapori katika maeneo yao na kuwa wakweli katika kutoa taarifa za kiwango cha uharibifu.

 ' Jana kuna mwananchi ametupigia simu kuwa tembo wamevamia shamba lake na kuharibu hekari nane,tumeenda pale tumekuta kiwango cha uharibifu alicho sema mtoa taarifa ni tofauti na hali halisi lakini pia alifyeka sehemu ya shamba lake yeye mwenyewe ili apate fidia' amebainisha Tutuba. 

Kwa Upande wake Afisa Wanyamapori Mkuu wa wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Antonia Raphael amewataka askari wanao patiwa mafunzo kufuatilia vyema mbinu na mafunzo wanayopewa huku akibainisha kuwa ushiriki wa wananchi katika kutoa taarifa utaifanya kazi hiyo iwe rahisi. 'Ninyi wananchi ni kiungo muhimu sana katika mapambano haya ,mtoe ushirikiano kwa wakufunzi. 

Amesisitiza Antonia. Katika hatua nyingine, Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Janemary Ntalwila amesema mkakati huo wa mafunzo shirikishi ni endelevu kwa maeneo yote yenye changamoto ya wanyamapori.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: