Vijana wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maandamano katika sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake ndani ya siku 100.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Baraka Shemahonge wameshiriki katika maadhimisho ya siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.  Philemon Sengati.

Sherehe za siku 100 za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika leo  katika viwanja vya Zima moto mjini Shinyanga, na kuhudhuriwa na wananchi, wakuu wa wilaya, madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa, pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwamo UVCCM.

Akizungumza kwenye sherehe hizo,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.  Philemon Sengati amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uwezo wake mkubwa kuliongoza taifa ndani ya siku 100, ambapo ameonekana kuwa na maono mazuri ya kuipeleka nchi kwenye uchumi mzuri, pamoja na kuwaletea maendeleo Watanzania.


 Amesema Rais Samia ni kiongozi ambaye ana maono mazuri ya kulifikisha taifa mbali, pamoja na kuwaletea maendeleo Watanzania, ambapo katika kipindi chake cha utawala ndani ya siku 100 amefanya mambo makubwa.

“Serikali mkoani Shinyanga tumeandaa sherehe hii ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani, sababu ni Rais wa kwanza Mwanamke hapa nchini, na ni Rais Mwanamke Afrika nzima, na amefanya mambo makubwa sana ndani ya siku zake 100, na sisi kama wasaidizi wake tuna ahidi kumuunga mkono kuwatumikia wananchi,”amesema Dk. Sengati.

“Hivi karibuni tumeshuhudia utiaji saini wa mradi mkubwa wa bomba la Mafuta, mradi wa Reli ya kisasa (SGR), pia amepunguza makato kwenye ufungiwaji huduma za umeme, faini za bodaboda, bajaji, kupunguza kodi kwenye nyasi bandia ili kuboresha viwanja vya michezo, kaongeza fedha uboreshaji miundombinu ya barabara na mambo mengi tu kufanya,”ameongeza.

Pia Dk. Sengati amewaahidi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuwaletea maendeleo, na kuwainua kiuchumi kwa kuongeza pato la mtu mmoja, kutoka kwenye Sh. Milioni 1.9 hadi Milioni 2 kwa mwaka , pamoja kuongeza uchangiaji wa pato la taifa kutoka Trilioni 8 hadi 10, na kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanakuwa na maisha mazuri na makazi bora.

Katika hatua nyingine amesema ataimarisha usalama wa mkoa, kupanua wigo wa mapato, kusimamia matumizi sahihi fedha za mlipa kodi ili utekelezaji wa miradi ya maendeleo iendane na thamani ya fedha, kuboresha usafiri, kujenga uwanja wa ndege, pamoja na kuondoa urasimu kwa wawekezaji, huku akiwataka watanzania kuchapa kazi ili kumuunga mkono Rais Samia kwa vitendo, pamoja na kuwa wazalendo.

Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema Rais Samia kwa kipindi kifupi ndani ya utawala wake fursa nyingi zimefunguka, pamoja na kutoa fedha nyingi kutekeleza miradi, ambapo katika bajeti ya 2021-2022 kila jimbo ametoa Sh. Bilioni Moja kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amesema Rais Samia ni mchapakazi mzuri na mpenda maendeleo, ambapo katika wilaya hiyo ametoa kiasi cha fedha Sh. Milioni 150 kujenga Zahanati ya Kitangili, Rubaga, na Oldshinyanga, na kutoa tena Sh. Milioni 428 kujenga daraja linalounganisha Kitangili na Chamaguha, pamoja na Sh. Milioni 53 kujenga madarasa na matundu ya choo shule ya Sekondari Ngokolo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, amesema umoja huo unamuunga mkono Rais Samia kwa asilimia zote, na atakayeonekana kwenda kinyume naye watamzingua, ambapo pia amekuwa akitetea vijana na kutoa ajira kwa wingi.

Amesema katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) utatoa ajira 11,000 kwa vijana, Bomba la Mafuta ajira 15,000, pia vijana 6,000 wamepata ajira ya ualimu, huku vijana wengine wakinufaika na mikopo ya Halmashauri asilimia Nne na kuinuka kiuchumi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga DK. Philemon Sengati, akizungumza kwenye sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM mkoani Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake
Mfanyabiashara mkoani Shinyanga Gilitu Makula, akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake, kwa kujali wafanyabishara na kuondoa utumiaji nguvu wa kudai kodi.
Mwenyekiti wa baraza la watoto Tanzania Nancy Kasembo,akizungumza kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Shinyanga Baraka Shemahonge, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemoni Sengati (kulia) kwenye sherehe hizo za kumpongeza Rais Samia kwa kuliongoza vizuri Taifa ndani ya siku 100 za utawala wake.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, wapili kutoka kulia, akiwa na Katibu wake Muhsin Zikatim, kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
Wanachama na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM, wakiwa kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.

Vijana wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maandamano katika sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuliongoza Taifa vizuri katika uongozi wake ndani ya siku 100.
Vijana wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maandamano katika sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri katika uongozi wake ndani ya siku 100.
Vijana wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maandamano katika sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri, katika uongozi wake ndani ya siku 100.
Burudani zikitolewa kwenye sherehe hizo.
Burudani zikiendelea kutolewa.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiongoza burudani kwenye sherehe hizo za kumpongeza Rais Samia.

Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Sherehe za kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliongoza Taifa vizuri ndani ya siku 100 za utawala wake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akiwa kwenye banda la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, na kuwataka waboreshe huduma zao kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemoni Sengati,akiwa kwenye banda la Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) na kuwataka waboreshe huduma zao kwa kusambaza maji kwa wananchi.
Hapa ni katika banda la Wakala wa maji Vijijini Ruwasa, katika sherehe hizo za kumpongeza Rais Samia.
Share To:

Post A Comment: