Mkurugenzi wa uthibiti ubora kutoka shirika la viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akitoa mafunzo kwa mawakala wa forodha na wafanyabiashara wa mahindi nanafaka nyingine juzi Katika mpaka wa Namanga  wilayani Longido mkoani Arusha

Na Woinde Shizza , ARUSHA 


Zaidi ya tani za mahindi elfu 10000 zimeshapitishwa katika mpaka wa Namanga uliopo wilayani Longido baada ya kuwepo kwa mkwamo upitishaji wa mahindi kwenda Katika nchi jirani ya Kenya kumalizika kutokana na viongozi wa nchi zote mbili kukaa na kukubaliana.


Ikumbukwe kuwa hivi karibuni nchi  ya Kenya ilipiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda kutokana na kile kinachoelezwa kwamba mahindi kutoka nchi hizo mbili sio salama kwa matumizi ya binadamu hali iliopelekea biashara hii ya mahindi kuzorota.

Hayo yamebainishwa n mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alipokuwa akifungua mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Namanga wilayani Longido  Mkoani Arusha  ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi mafunzo yalioandaliwa na shirika la viwango  Tanzania (TBS).

Alianza kwa kumpongeza Rais Samia Suluhu kwa kuweza kutatua tatizo hilo na kubainisha kuwa kwa sasa biashara ya usafirishaji wa mahindi imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana na hadi sasa zaidi ya tani efu kumi za mahindi zimeshapitishwa kwenda nchi jirani ya Kenya kupitia mpaka wa Namanga.

Alisema kuwa pamoja na hayo kumetokea matatizo mbalimbali ambayo yamebainika yanatokea Katika nchi yetu huku ikiwemo tatizo kubwa tulinalo la baadhi ya mahindi yetu kukutwa na simu kuvu  pia tatizo la namna ya kufungasha mahindi kwa ajili ya usafirishaji pamoja na namna ya kufanya lebo hali iliopelekea baadhi ya mahindi yetu kurejeshwa nchini.


"Labda nipongeze TBS kwani walivyogundua tatizo hilo wameamua kuwapa semina wafanyabiashara hawa  ya namna ya kuhundua mahindi yenye sumu kuvu pia niwashauri wasiishie hapa tu bali waende na kule ambapo mahindi haya yanazalishwa nikimaanisha kuanzia kitoa elimu kwa mkulima wa chini hadi kufikia wauzaji wadogo na wakubwa ili tatizo hili liweze kuisha na tuweze kuzalisha kwa wingi bidhaa zenye tija ambazo tutaziuza kimataifa na kujiongezea kipato"alisema Mwaisumbe.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga amesema wafanyabiashara hawana budi kuhakikisha mahindi wanayonunua kama yamezingatia kanuni bora za kulimo ili kuzuia fangasi wanaoweza kusababisha sumu kuvu kwenye mahindi.

Alisema wafanyabiashara hao wanatakiwa kujua mahindi wanayokuwa wakinunua yanayotoka wapi ili kuweza kuepuka hasara inayoweza kujitokeza pindi mahindi yatakapokuwa na sumu kuvu.

“Ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kujua Mahindi wanayoyanunua yanazalishwaje kwani ni muhimu sana kujua yule anayekuuzia mahindi kwa lengo la kujua kama anafuata kanuni bora za kilimo kutokana na kwamba inakupa uhakika na ukinunua haitaleta shida kwenye usafirishaji”Alisema Msasalaga.

“Mafunzo haya yatawasaidia wafanyabiashara namna ya mahindi yanavyopokelewa,kuna taratibu za kupeleka mahindi nje ya nchi na kila nchi ina namna ya kulinda usalama wa chakula kwa   wananchi wake”alisema Msasalaga.

Akielezea namna ya sumu kuvu unaweza kuepukika,Msasalaga amesema ni lazima kanuni bora za usindikaji wa mahindi na mnyonyoro mzima wa uzalishaji uwe umefuatwa huku akiwataka wafanyabiashara wafuate taratibu ambazo zinatakiwa kwa kuwa nchi inayopokea bidhaa ndio inayotoa sharti ya kupokea mizigo.

Kwa upande wake afisa usalama wa vyakula kutoka TBS dkt Candida shirika alisema kuwa simu kuvu inayopatikana inapatika Katika baadhi ya mazao ya nafaka Kama mahindi ,karanga na mengineyo lakini mahindi ndio yanashambuliwa kwa kiasi kikubwa.


Alisema sumu kavu inaikiwa nyingi na akatumia binadamu unaweza kumletea madhara makubwa Kama vile kusababisha  saratani ya ini ,kupunguza kinga za mwili,udumavu kwa watoto,pamoja na saratani ya Koo.

Semina hiyo imefanyika katika Mikoa mitatu ambayo ni mpaka wa Holili mkoani Kilimanjaro,Namanga Mkoani Arusha na Horohoro Mkoani Tanga.



Share To:

Post A Comment: