Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro,akizungumza na Waislamu  katika dua ya arobaini ya Sheikh Mohamed Makula iliyofanyika Iguguno wilayani Mkalama mwishoni mwa wiki. 

Sheikh wa Wilaya ya Singida Issa  Simba,akizungumza kwenye dua hiyo.

Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Dua ikiendelea.
Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Mohamed Makula.

 Wakina Mama wakiwa katika Arobaini ya Marehemu Mohamed Makula.

Dufu likipigwa  katika mkutano huo.

Picha zikipigwa.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akiongoza kuomba dua kwenye arobaini hiyo.
 Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan Mlau  akizungumza katika dua hiyo.

Utambulisho ukifanyika.
Walimu wa dini wakitambulishwa.
Utambulisho ukifanyika.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata)  Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii, akizungumza katika dua hiyo.
Sheikh wa Kata ya Mungu Maji, Juma Sungi, akizungumza katika dua hiyo.
Sheikh wa Wilaya ya Mkalama,Miraji Miraji, akizungumza katika dua hiyo.
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro, akisalimiana na Waislamu waliofika kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Singida Mjini, Sheikh Hamisi Kisuke,akizungumza katika dua hiyo.
Mwenyekiti wa Bakwata Wilaya ya Mkalama, Muadh Musa Ntoga, akizungumza katika dua hiyo.

Dua katika arobaini ya Marehemu Mohamed Makula, ikiendelea.


 Na Dotto Mwaibale, Singida


KAIMU Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro amemtangaza Sheikh Shabani Mkanga kuwa Kadhi wa mkoa huo kuanzia sasa.

Sheikh Nassoro alitoa tangazo hilo katika dua ya arobaini ya Sheikh Mohamed Makula iliyofanyika Iguguno wilayani Mkalama mwishoni mwa wiki.


" Muda mchache tangu tuanze dua hii ya Mzee wetu Makula Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania  (BAKWATA) Mkoa wa Singida Sheikh Burhan Mlau amenipa nakala ya uteuzi wa Sheikh Shabani Mkanga kuwa umekamilika sasa ndio Kadhi nikiwa kama Kaimu Sheikh wa mkoa nimeipokea hiyo nakala na mbele ya shughuli hii namtangaza rasmi kuwa Kadhi wa Mkoa wa Singida na ninakuagiza Katibu wangu  Sheikh Mlau kuanzia sasa ufanye kazi na kadhi huyo mteule," alisema Nassoro.

Alisema kesi zote zilizokwishafunguliwa sasa zielekezwe kwa Sheikh Shabani Mkanga na si vinginevyo na aliyekuwepo kwenye nafasi hiyo sasa ataitwa kadhi mstaafu na hana mamlaka ya kufanya kazi hiyo tena.

Alisema mambo hayo ndio yanayotakiwa kufuatwa na Waislamu kwani mamlaka za juu zimemteua na wao wajibu wao ni kumsikiliza na ku mfuata.

Sheikh Nassoro alitumia nafasi hiyo kuwaomba waislamu wafike mahala waseme migogoro sasa basi kwani wana migogoro mingi ambayo haina tija na kuwa haiwafai.

"Tuna fursa nyingi tunaziacha ambazo wajibu wetu kuzitumia lakini hatuzitumii, wasio na migogoro wanazitumia fursa hizi moja ya fursa ambayo nataka Waislamu wa Mkalama waitumie ni eneo la uwanja lililotangazwa wakati wa mazishi ya Sheikh Makula kuwa ufanyiwe kazi na kwa kuwa viongozi wote mpo hapa natoa agizo kuwa uwanja huo ujengwe chuo au Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ikiwa namna ya kumuenzi marehemu na ipewe jina lake," alisema Nassoro.

Alisema wamuenzi mzee huyo kwa kuweka alama na watu waanze ujenzi kwa kutumia fursa ya ujenzi huo kama wanavyotumia wenzao wa kristo misamaha ya kodi ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi ambayo waislamu hawaitumii hasa wanapo jenga misikiti na madrasa zao wampelekee Katibu wa Bakwata barua za maombi hayo badala ya kumpelekea barua za majungu na vitina ambazo zimejaa ofisini kwa katibu huyo.

Aidha Sheikh Nassoro aliwataka waislamu wa Msikiti wa Mariam Iguguno aliokuwa akiongoza Sheikh Mohamed Makula kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na mchakato wa kumpata Sheikh mwingine na pindi atakapopatika atakaye teuliwa na mamlaka husika wampe ushirikiano.

Share To:

Post A Comment: