Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya alikuwa kiongozi mwenye maono adhimu na ya mbali. Aliamini katika uongozi wenye kujali tija na matokeo. Nje ya uongozi alikuwa mfugaji hodari. Alikuwa kada mtiifu wa CCM na msimamizi asiyechoka wa sera za CCM.

Alikuwa msema kweli na mtu mwenye uthubutu. Kwa wale tuliokua nae katika kipindi chake cha ubunge, hatutasahau umakini wake, wa kutumia kanuni kuiamsha serikali pale inapolala. Ni msimamo wake thabiti uliosababisha abatizwe jina la 'mzee wa mabomu'.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

Edward Ngoyai Lowassa.
Waziri Mkuu wa zamani
Share To:

Post A Comment: