Na Lucas Myovela_ Arusha.

Katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Antony Sanga amesema kuwa iwapo wadau na jamii kwa ujumla wasiposhirikiana katika utunzaji wa rasilimali za maji  siku za usoni kutakuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji.

Mhandisi Sanga aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa Jukwaa la Bonde la Pangani  unaoendelea Mkoani  Arusha  ambapo alisema kuwa maziwa na mito haviongezeki lakini watu wanaongezeka hivyo wanapaswa kutathimini baada ya Mika 50 hali ya upatikanaji wa maji itakuwaje.

“Kwasasa tupo milion 60 na maji tunayoyatumia vyanzo haviongezeki hivyo tunapaswa kuutunza vyanzo kwaajili ya sasa na vizazi vijavyo na ni wajibu wa kila mmoja kushiriki katika kutunza rasilimali za maji,”Alisema Mhandisi Sanga.

Ameeleza kuwa wananchi waelimishwe wasilime kwenye vyanzo vya maji, wasikate mito, wasitiririshe maji machafu kwenye mito na mengine mengi yanayoleta uharibifu wa vyanzo ambapo pia alisema kuwa wanawahitaji na wanawategemea wadaukatika suala hilo ili kuhakikisha vyanzo vinalindwa kwa manufaa ya sasa na baada.

 Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya maji bonde la mto Pangani Mhandisi  Segule Segule alisema kuwa lengo kubwa kushirikishana na kubadishana uzoefu wa kutunza rasilimali za maji katika mabonde   pamoja na kujadili changamoto zilizopo ili kuweza kutoka na mkakati utakaoendeleza mabinde ya maji.

Mwenyekiti wa majukwaa ya maji taifa Mhandisi Mbogo Futakamba alisema kuwa jukwaahilo linasaidia kuwa na vikundi kazi ambavyo vinasaidia upatikanaji wa maji na kutatua migogoro.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa rasilimali za maji Dkt George Lugomela alisema kuwa suala la kushirikisha wadau wa maji katika usimamizi wa rasilimali za maji  ni la kiserq ambapo kwa kutambua kuwa maji no rasilimali yenye ukomo ni muhimu kusimamia kwa weledi na umakini mkubwa.

Dkt Lugomela alieleza kuwa watu wamekuwa wakiongezeka na kufanya matumizi ya maji kuwa makubwa kwa mtu mmoja ambapo upatikanaji wa maji kwa mtu mmoja umeshuka kutoka 2600 na kufikia 2200.

Alifafanua kuwa lengo kubwa ni kujenga uelewa wa masuala ya rasilimali za maji kwani ni haki ya kula mtu kuyatumia lakini kwa kufuata sheria ambapo kama mtu anachota kwa kutumia ndoo ni Tulsa lakini kama mtu anataka kufunga miundombinu ni lazima awe na kibali.

Naye katibu tawala wa mkoa wa Arusha Athumani Kihamia alisema kuwa huwezi kuzungumzia maendeleo ya sekta yoyote ikiwemo viwanda bila kuzungumzia maji hivyo mkutano huo una umuhimu sana katika mustakabali wa nchi na anaamini yatayoenda kujadiliwa yatakuwa na tija katika kuendeleza mabonde.

Hata hivyo mkutano huo wa siku mbili umebeba kauli mbiu isemayo“ utunzaji wa vyanzo vya maji ni jukumu letu sote”

Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: