Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja ameelezea mikakati ya kukabiliana na Wanyamapori wakali na waharibifu wanaovamia maeneo ya makazi na kusababisha adha kwa wananchi.
Akizungumza leo na wakazi wa Wilaya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mhe. Masanja ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kupanda miti kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi, kuweka mizinga ya nyuki ambayo itasaidia kuzuia tembo kuingia katika maeneo ya Wananchi.
Katika hatua nyingine Mhe.Masanja amewaonya wafugaji wanaoingiza mifugo Hifadhini kuacha tabia hiyo mara moja kwani ni moja ya sababu inayochochea tembo kutoka nje ya Hifadhi kwa vile Tembo hawawezi kuvumilia kuishi pamoja na ng'ombe, Hivyo ng'ombe wamekuwa ni kisababishi cha tembo kuvamia mashamba na kuleta madhara kwa wananchi.
Post A Comment: